Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeyaonya mashirika ya umma endapo hayatafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato yatafutwa mara moja na wafanyakazi wake kuwatafutia sehemu nyingine za kazi.

Waziri anaeshughulikia fedha, uchumi na mipango ya maendeleo Omar Yussuf Mzee amesema lengo la kuanzishwa mashirika ni kuleta faida na sio kuitia hasara serikali hivyo endapo mashirika hayo hayatafanya vizuri wizara yake itapendekeza yafutwe.

Akizungumza na wahasibu wakuu na wakaguzi wa ndani wa taasisi za serikali na mashirika ya umma huko hoteli ya Bwawani waziri Mzee amesema Zanzibar ilikuwa na mashirika mengi, lakini yamefutwa baada ya kuitia hasara serikali kwa kutozalisha kwa faida

Aidha waziri Mzee amewataka wahasibu hao kusimamia mapato ya serikali kutokana na kuwepo taarifa kwa baadhi ya watendaji kuhushi risiti zinazotolewa na serikali na kuzitoa kwa wananchi.

Amesema endapo vitendo hivyo wataendelea kuvifumbia macho ukusanyaji wa mapato ya serikali utapungua na kutupiwa lawama wizara ya fedha

Miaka kadhaa iliyopita serikali imeyafuta mashirika yake kadhaa yaliokuwa hayazalishi kwa faida likiwemo shirika la viwanda, shirika la biashara BIZANJE

Advertisements