Baraza la wawakilishi

Kikao cha baraza la wawakilishi kinachokabiliwa na shindikizo la kutoujadili muswada wa sheria wa utumishi wa umma kutoka kwa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Zanzibar ZATUC kitaanza leo

Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa ZATUC Khamis Mohammed ametaka mswada huo ufanyiwe marekebisho kabla ya kujadiliwa na barazani kwa kile anachodai hauna maslahi kwa wafanyakazi.

Ametaja baadhi ya kosoro zilizomo kwenye muswada huo ni kutotoa haki ya wafanyakazi kuandamana pamoja na kuipa madaraka makubwa katibu mkuu kiongozi.

Mohammed amedai mswaada huo pia unapinga na sheria za kazi namba 11 ya mwaka 2005 ambapo amesema suala hilo litaleta utata kwa wafanyakazi wanapodai haki zao.

Hata hivyo Shirikisho hilo limewaomba wajumbe wa baraza la wawakilishi wasipitishe mswaada huo hadi utakaporudishwa tena kwa wahusika ili waufanyie marekebisho zaidi.

Kikao hicho cha baraza la wawakilishi pia kitajadili muswada wa sheria ya masharti ya uwekezaji na usimamizi wa viwango za bidhaa pamoja na kuzifanyia marekebisho baadhi ya kanuni za baraza hilo kutokana na kuwepo mfumo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Akizungumza na wandishi wa habari kuelezea matayarisho ya kikao hicho katibu wa baraza hilo Ibrahim Mzee Ibrahim amesema kanuni ziliopo sasa haziwezi kufanya kazi hasa baada ya kuondolewa wakuu wa mikoa kuwa wajumbe wa baraza hilo na kiongozi wa kambi ya upinzani…

Kikao hicho pia kitapata fursa ya kujadili na kuipitia hutuba ya ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein aliyoitoa katika kikao cha ufunguzi wa baraza hilo Novemba 11, mwaka jana na kufanya uchaguzi wa Naibu Spika, wenyeviti wawili na uchaguzi wa wajumbe watatu watakaoingia katika kamati ya uundwaji wa bajeti katika baraza la wawakilishi.

Advertisements