Wanafunzi wa chuo kikuu cha taifa Zanzibar SUZA wakiwa katika mahafali

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imemtaka mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa kuthibitisha madai yake kwamba bodi ya mfuko wa elimu ya juu Zanzibar inaendeshwa kwa vitendo vya rushwa.

Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zahra Ali Hamad ametoa wito huo alipokuwa akijibu suala la mwakilishi huyo aliedai bodi hiyo inahusika na rushwa wakati inapotoa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu.

Amesema iwanawezekana Jussa anazotaarifa juu ya vitendo hivyo na kumtaka kushirikiana na wizara kwa kutoa ushahidi juu ya afisa yoyote anaehusika na rushwa katika utowaji wa mikopo kwa wanafunzi.

Zahra ameahidi endapo mtendaji yoyote atabainika kufanya vitendo vya rushwa  serikali haitamuonea haya na badala yake kumfikisha mahakamani

Hata hivyo Naibu waziri huyo amekiri wanafunzi wanaosoma nje ya Zanzibar hawapatiwi fedha kwa ajili ya makaazi na chakula kutokana na uwezo mdogo wa kifedha unaoikabili serikali.

…..2…ZANZIBAR……

ZANZIBAR……2….

Mwaka wa fedha 2010/2011 bodi ya mfuko wa elimu ya juu Zanzibar iliomba kutengewa shilingi bilioni 4.5, lakini serikali ilidhinisha shilingi bilioni 2.5 na hadi kufikia sasa shilingi bilioni 1.19 sawa na asilimia 47.6 ndizo zilizoingizwa.

Kwa mujibu wa naibu waziri huyo wanafunzi elfu moja 349 wakeimwemo wanawake 745 wamepatiwa udhamini wa masomo ya elimu ya juu na serikali ya mapinduzi Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

Advertisements