Utowaji wa huduma za kupima kisukari

Jumla ya wagonjwa 62 walioguwa ugonjwa wa kisukari Zanzibar wamekatwa viungo kati yao 24 wamefariki dunia katika kipindi cha mwaka 2009/2010.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri wa afya Dr. Sira Ubwa Mwamboya amesema tatizo hilo linatokana na wagonjwa wengi wa kisukari kuchelewa kufika hospitalini na inapofikiwa uwamuzi wa kukatwa kiungo sumu imesambaa mwilini.

Hata hivyo amesema suala la wagonjwa wanaofariki dunia wakiwa matibabuni halitokana na ukosefu wa madaktari, lakini inategemea mgonjwa anavyoidhibiti sukari yake

Aidha Dr. Mwamboya wamewataka wananchi kujitokeza kupima afya zao mara kwa mara ili kujiepusha na maradhi kama hayo.

Kuanzia mwaka 2009 hadi 2010 jumla ya wagonjwa elfu tatu, 286 walihudumiwa katika kliniki za Unguja na Pemba kati yao wagonjwa 464 walikuwa wapya.

 

Advertisements