Mohammed Ghailan

Familia ya mtanzania aliehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na kosa ugaidi imeziomba serikali za Tanzania kusaidia mtoto wao Ahmed Ghaila apunguziwe adhabu na jalada lake kupitiwa upya.

Ghailan ambae ni mzanzibari alipatikana na hatia ya kuhusika na mashambulizi katika balozi za Marekani mjini Dar es Salaam na Nairobi Kenya mwaka 1998.

Mama mzazi wa Ghailan, Bimkubwa Said amesema ameshutushwa kwa kiasi kikubwa na hukumu hiyo na kuziomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar na serikali ya muungano kusaidia juu ya adhabu hiyo.

Hata hivyo amesema amefurahishwa na kauli ya mawakali wa mwanawe kukata rufaa juu ya hukumu hiyo

Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004 na kupelekwa kwenye kambi ya siri inayosimamiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, Cuba, mwaka 2006 na baadaye alihamishwa mjini New York alikoshtakiwa

Katika mashambulio hayo anayohusishwa Ghailan zaidi ya watu 224 walifariki dunia na wengine kadhaa walijeruhiwa.

Ghaila amekuwa mfungwa wa kwanza katika jela ya Guantanamo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia.

Advertisements