Ali Khatib Katibu mkuu TADEA

Baadhi ya vyama vya siasa Zanzibar vimeiomba serikali kutekeleza ahadi yake ya kumaliza migogoro ya ardhi nchini kwa njia ya amani badala ya kuwa chanzo cha migogoro.

Wakizungumza na mmiliki wa blogi hii juu ya kauli ya serikali ya kutaka kumaliza migogoro ya ardhi, viongozi wa vyama vya siasa vya A.F.P na TADEA wamesema wengi waliopewa viwanja wana haki kama wazanzibari.

Mwenyekiti wa A.F.P Saidi Soud amesema watu wengi waliopewa maeneo ya ardhi wamepewa kihalali na kuiomba serikali kuwandama wale wananchi waliochukua maeneo ya ardhi kwa nguvu.

Amesema ana amani serikali iliyopo madarakani inaweza kumaliza migogo ya ardhi endapo haitawaonea haya wale

aliowataja vigogo waliopora ardhi za wananchi

Said Soud-A.F.P

Nae katibu mkuu wa chama cha TADEA Juma Ali Khatib amepongeza kauli hiyo ya makamo wa pili wa rais wa Zanzibar aliyoitoa katika kikao cha baraza la wawakilishi na kusema inahitaji utekelezaji isiwe ahadi tupu.

Amesema serikali imeshatoa kauli kadhaa bila ya kutekelezaj na kutaka kuigwa mfano wa waziri Ana Tibaijuka katika kumaliza migogoro ya ardhi huko Tanzania bara.

Amesema wananchi wanyonge amechukuliwa ardhi zao na wale aliowaita vigogo wa serikali, hivyo kuwepo kauli hiyo inahitaji kutekelezwa na uongozi wa halmashauri za wilaya

Jana makamo wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiahirisha kikao cha baraza la wawakilishi amesema migogoro mingi ya ardhi inayowahusu wananchi wa kawaida walioporwa ardhi zao wanazozitumia kwa kujikimu haijatatuliwa  .

Amesema hakuna hata mkoa mmoja kati ya mitano ya Zanzibar, uliokuwa haujakumbuwa na mgogoro wa ardhi na kusema serikali itachukua juhudi za kumaliza migogoro hiyo kati ya walalamikaji na wanaolalamikiwa

Advertisements