Mji mkongew wa Zanzibar

Wakaazi wa maeneo ya Mji Mkongwe wamezilalamikia baa katika maeneo ya mji huo kwa kuendelea kuuza vileo licha ya kuzuiwa na mahkama ya vileo ya Mwanakwerekwe.

Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya waandishi wa habari huko mtaa wa Vuga ilipo baa ya Dharman Tang inayolalamikiwa.

Wakaazi hao wameiomba serikali kuzuwia baa zilizomo kwenye mji mkongwe kuendesha biashara za vileo

Aidha wakaazi hao wametishia kuishitaki bodi inayopitisha leseni za vileo. Sheria iliyopo tokea utawala wa kikoloni  ya mwaka 1828 inazitambua kuwepo kwa baa saba Unguja ambazo zilikuwa nje ya mji wa Zanzibar.

Hivi karibuni watu wasiojulikana wamezita moto baa mbili za maeneo ya Chumbuni na mwanyanya kwa madai yakuendesha shughuli zao kwenye makaazi ya watu

Advertisements