Naibu katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Saleh Ramadhan Ferouz amesema tokea kuzaliwa kwa chama hicho miaka 34 iliyopita kimepata mafanikio ikiwemo kuendelea kushika madaraka ya nchi.

Akizungumzia mafanikio ya chama hicho tokea kuzaliwa mwaka 1974 amesema CCM pia kimesaidia ujenzi wa demokrasia wa kuingia mfumo wa vyama vingi kutoka chama kimoja hatua aliyosema ilikuwa ngumu.

Kuhusu uchumi amesema chama hicho kimepata mafanikio katika kujenga na kusimamia uchumi wa Tanzania kwa kuanzisha sera zenye mwelekeo za serikali zote mbili katika kuleta maendeleo ya kiuchumi.

Feroudh amesema ikilinganishwa na miaka 34 iliyopita, hali yakipato cha wananchi inaendelea kuimarika kwa kujenga makaazi bora, kuongezeka uwekezaji na huduma za kijamiiĀ 

Sherehe za miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM katika mkoa wa mjini magharibi zitaanza kwa maandamano na kufuatiwa mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na mjumbe wa kamati kuu ya CCM na rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein huko uwanja wa Kisonge.

Wakati huo huo maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM kitaifa yatafanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi katika sherehe hizo anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa CCM rais Jakaya Kikwete.

Katibu mkuu wa CCM Yussuf Makamba amesema maadhimisho hayo pia yatatumiwa katika kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita

Chama cha Mapinduzi CCM kilizaliwa mwaka 1974 baada ya kuanganishwa vyama vya Afro Shirazi na TANU katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Amani mjini Zanzibar.

Advertisements