Baa nyingine imechomwa moto usiku wa kumkia leo katika manispaa ya mji wa Zanzibar ukiwa umeteketeza mali zote zilizokuwemo ndani ya baa hiyo.

Akizungumza na Zenji Fm Radio mmilikiwa wa baa hiyo ya Crist Garden iliyopo mtaa ya Sokomhogo, eneo la Mji Mkongwe Cristopher Jon Makata amesema baa hiyo imetiwa moto majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo.

Amesema mali zote zilizokuwemo ndani ya baa zinazokisiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50

Amesema kutokana na kitendo hicho ameiomba serikali kulifatilia kwa kina suala hilo ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Makate amesema endapo wahusika hawatachukuliwa hatua za kisheria watafanya maovu zaidi.

Nae mkaazi wa eneo hilo Khalid Said Suleiman amesema si jambo la busara kwa wananchi kuchukua sheria mikononi mwao.

Hata hivyo ameiomba serikali kutochelewesha kesi za madai zinazofunguliwa na wananchi wanaopinga kuwepo kwa baa katika maeneo yao wanayoishi

Hii ni baa ya tatu katika mkoa wa mjini magharibi kuchomwa moto na watu wasiojulikana katika kipindi cha wiki mbili kwa kile kinachoelezwa baa hizo ziko karibu na makaazi ya wananchi na kuendesha vitendo viovu

Advertisements