Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM taifa rais Jakaya Kikwete amesema hatasita kuichukulia hatua kampuni ya Dowans inayotaka kulipwa mamilioni ya shilingi iwapo taratibu zitmhijati kufanya hivyo.

Akizungumza kwa mara ya kwanza juu ya sakata la Dowans mjini Dodoma leo amesema yeye binafsi hana maslahi yoyote na kampuni hiyo kama baadhi ya watu wanavyodai.

Kikwete amesema hayo alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM mjini Dodoma.

Advertisements