Uwanja wa ndege wa Zanzibar

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imeombwa kuongeza nguvu katika kudhibiti uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya unaoendelea kuathiri maisha ya vijana.

Akizungumza na Zenji fm radio mkaazi wa Jangombe Abdalla Hassan amesema dawa za kulevya ziendelea kuumiza nguvu kazi ya taifa ambao ni vijana na kushauri serikali kulivalia njuga suala hilo.

Amesema dhana iliyojengeka wananchi wa kawaida wanawaficha watu wanaoingiza dawa za kulevya sio kwali, lakini vyombo vinavyohusika haviwajibiki ipasavyo kutokana na dawa hizo kuingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Hassan amefahamisha ulinzi dhaifu uliopo katika maeneo ya bandarini na uwanja wa ndege maeneo ambayo serikali inapaswa kuyadhibiti

Hata hivyo Hassan amesema watu wanaoingiza dawa za kulevya ni wa chache na wanaweza kudhibitiwa, lakini amedai ungizaji wa dawa hizo umetawaliwa na vitendo vya rushwa.

Advertisements