Bei za vyakula zinaendelea kupanda kwa kasi katika visiwa vya Unguja na Pemba na hivyo kuathiri maisha ya wananchi.

Kufuatia hali hiyo waziri wa bishara, viwanda na masoko Ahmmed Mazurui ana mpango wa kukutana na wafanyabishara kuangali jinsi gani wanaweza kupunguza bei hizo.

Tatizo hilo la kupanda bei ya vyakula limeonekana katika masoko mengi ya mji wa Zanzibar, huku wafanyabiashara wakidai vyakula vilivyoko katika mzunguuko wa biashara ni kidogo.

Mwezi uliopita kikao cha baraza la wawakilishi kilipitisha mswada wa sheria pamoja na mambo mengine ulizingatia udhibiti wa bei za bidhaa.

Hivi karibuni mkuu wa Benki ya Dunia Robert Zoellick amesema dunia unakabiliwa na ongezeko kubwa la bei za vyakula na kuyataka mataifa duniani kuchukua hatua ili kukabiliana na ongezeko hilo.

Kwa mujibu wa takwimu za dunia bei za vyakula hivi sasa zimepanda katika nchi nyingi duniani ikilinganishwa na kupanda kwa bei hizo mwaka 2007 na 2008.

Advertisements