Wanafunzi wa elimu ya juu wakiandamana kupinga ucheleweshaji wa mikopo yao unaofanywa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu Tanzania

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameteuwa tume ya watu kumi na moja itayochunguza na kutoa mapendekezo ya kuimarisha kazi za bodi ya utowaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Bodi hiyo katika siku za karibuni imekuwa ikilalamikiwa na wanafunzi kwa madai ya kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Akitangaza uwamuzi huo wa rais Kikwete waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tume hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha siku 60 kuanzia Februari 14  hadi April 15 mwaka huu na itaongozwa na makamo mkuu wa chuo cha Dar es Salaam taaluma Profisa Makinya Maboko

Advertisements