Mizengo Pinda

Balozi Seif Idd

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wamepongezwa kwa ukaribu wao na ushirikiano mzuri wanaoutoa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha Tanzania.

Hayo yalielezwa na Wajumbe wa Tume hio katika mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi alipokutana nao hapo Afisini kwake Vuga.

Akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa tume hiyo tokea kuanzishwa kwake Menyekiti wake Mhe Willium Shelukindo alisema tume hio tokea uanzishwa kwake mwaka 2003 imeshafanya utafiti wa mambo kadhaa na kutoa mapendekezo ya utekelezaj wake katika Serikali zote mbili.

Aliyataja kati ya mambo muhimu waliyokwisha amuliwa ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya vigezo vya kugawana mapato ya Muungano kwa Serikali za Zanzibar na Serikai ya Mungano wa Tanzania.

Halikadhalika Mwenyekiti huyo alieleza changamoto zinazoikabili tume hiyo ikiwa ni pamoja na kutokuwepo na utaratibu madhubuti wa kushughulikia ushauri unaotolewa na tume hiyo.

Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais Mhe Balozi Seif Ali Iddi alisema Tume hiyo ni muhimu sana na kwa kuwa kuwepo kwake kutasidia majibu mengi ya kero za Muungano na kuweka wazi masuala ya mapato yake.

Alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ye Zanzibar imeyapokea mapendekezo yote yaliyowasilishwa na tume hiyo na imeshayafanyia kazi na kutoa ushauri wao. Wanasubiri wenzao SMT kutoa ushauri wao juu ya mapendekezo hayo.

Mheshimiwa Balozi Iddi aliihakikishia tume hiyo kuwa Serikali iko tayari wakati wo wote kuyapokea mapendekezo na ushauri wao kwa maslahi ya pande mbili za Jmhuri ya Muungano wa Tanzania

Advertisements