Archive for March, 2011

Makamu II wa rais Zanzibar akutana na rais wa Iran

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi ameeleza haja ya Serikali mbili baina ya Iran na Zanzibar kuangalia upya makubaliano yao ya awali kwa lengo la kuyatafutia njia bora za utekelezaji wake.

Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyaeleza hayo katika mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Dk. Mahmoud AhmediNejad katika Ikulu ya mjini Tehran.

Mhe. Balozi Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na kuwa na makubaliano kadhaa yanayohitaji kutekelezwa ambayo mengi hayajafanyiwa kazi.

Hivyo alishauri kuundwa kwa Tume ya watu wachache ya kufanyia mapitio ya makubaliano yote na kukaa pamoja na wajumbe wa Serikali ya Iran kwa ajili ya kuyatafutia njia za kuyatekeleza.

Aidha, alieleza kufurahishwa kwake na nia ya Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuimarisha ushirikiano wao kwa kuanzisha Ubalozi Mdogo wa nchi hiyo hapa Zanzibar.

Halikadhalika aliwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein za kumtakia kheri katika sherehe za mwaka za jadi.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Dk. Mahmoud AhmediNejad alieleza kupendezewa kwake na salaam za viongozi hao wa Tanzania na kwa ujumbe wa Zanzibar kushiriki Tamasha hilo.

Alisema Iran na Zanzibar ni ndugu marafiki wa muda mrefu kutokana na historia ya utamaduni wao mambo ambayo yamezidi kuimarisha uhusiano baina yao na kuishauri Zanzibar kufanya maadhimisho kama haya.

Aidha, alikubaliana na mapendekezo na ushauri wa Makamu huyo wa Pili wa Rais wa Zanzibar ya kutafuta mbinu za kuanza utekelezaji wa makubaliano yao kwa haraka.

Kuhusu maadhimisho ya Jadi ya Mwaka wa Nowruz, Mhe. Dk. AhmediNejad amesema sherehe hizo zina madhumuni ya kuimarisha imani miongoni mwa jamii na kujenga mapenzi na umoja miongoni wao.

Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi tayari yuko Iran akimuwakilisha Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika maadhimisho ya Sherehe za mwaka za Iran.

Advertisements

PROFISA LIPUMBA AWATAKWA WANANCHI KUIHOJI SERIKALI KUPANDA GHARAMA ZA MAISHA

Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profisa Ibrahim Lipumba amesema serikali ya Mapinduzi Zanziar inahitaji muda zaidi wa kupunguza gharama za maisha kwa wananchi.

Amesema katika kipindi cha miezi minne bado ni kidogo kupima uwezo wa serikali wa kukabiliana na gharama za maisha na kuwataka wananchi kuvuta subra.

Hata hivyo Profisa Lipumba amewataka wananchi wasichoke kuihoji serikali yao juu ya azma yake ya kuleta maisha bora kwa kila mzanzibari.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Kibandamaiti amesema Zanzibar inafursa nyingi za kuendeleza uchumi ikiwemo shughuli za bandari, kilimo na sekta ya biashara na utalii

Prifisa Lipumba amesema anaimani serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar inaweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kutatua tatizo la ajira kwa vijana, hivyo amewataka wananchi kuendelea kuinga mkono.

Nae mwenyekiti wa chama cha NCCR-MAGEUZI taifa James Mbatia akizungumza katika mkutano huo amesema mabadiliko ya katiba yaliofanywa Zanzibar na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa yameleta changamoto kwa Tanzania.

Amesema maadiliko hayo ambayo pia yamegusa katiba ya jamhuri ya muungano Tanzania yamechochea kwa kiasi kikubwa kutaka kuandikwa kwa katiba mpya.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwashukuru wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa kuinga mkono wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana.

DENI LA NJE LA ZANZIBAR LAFIKIA BILIONI 152

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inadaiwa jumla ya shilingi bilioni 152, deni la nje na shilingi bilioni bilioni 42.8 deni la ndani.

Waziri wa nchi, afisi ya Rais, Feddha , uchumi  Mipango  ya Maendeleo Zanzibar, Omar Yusuf Mzee  amesema kiasi  kikubwa  cha deni  la taila  linatokana na mikopo  kwa matumizi ya mipango  ya miundo mbinu ya maji, barabara na sekta nyengine za maendeleo.

Akijibu suala la katika kikao cha Baraza la Wawakilishi  kuhusu msimamo   madeni ya serikali  amesema  madeni ya nje  hulipwa kwa kiwango cha  miaka 25 chini ya udhamini  wa serikali ya  Muungano, wakati  deni la ndani hulipwa kila mwaka kutegemea  uwezo wa  bajeti.

Amesema serikali inategemea mikopo na misaada  kutoka  kwa washirika wa maendeleo kutokana na  mahitaji  ya maendeo ya  nchi.

Wakati huo huo waziri wa viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui amesema zao la karafuu linakosa bei kutokana na kuhodhiwa na wafanyabiashara wa kati.

Waziri Mazurui amesema hayo alipokuwa akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea mjini hapa.

ZANZIBAR KUPATA UFADHILI WA UJENZI WA BANDARI KUTOKA OMAN

Eneo la Mpigaduri Zanzibar linalotarajiwa kujengwa bandari ya mizigo

Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar inatarajia kupata ufadhili wa ujenzi wa bandari huru na kuendeleza maeneo ya biashara kutoka nchi za falme za kiarabu.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kurejea akitokea nchi za Falme za kiarabu na Oholanzi amesema Dubai na Sharjah zimekubali kusaidia Zanzibar katika ujenzi wa mpya bandari na maeneo ya biashara huru.

Malim Seif amesema amezungumza na wafanyabiashara wakubwa wa nchi hizo pia kuangalia uwezekano wa kuwekeza Zanzibar ili kuisaidia kuimarisha uchumi wake.

Amesema serikali itafuatilia ahadi zilizotolewa na nchi hizo za kuisaidia Zanzibar kiuchumi ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo inafanikiwa

Amesema kwa upande wa serikali itahakikisha inaweka miundo mbinu itakayosaidia kuweka mazingira mazuri ya miradi ya kiuchumi, huku ikijua miradi hiyo inahitaji fedha nyingi.

Aidha Malim Seif amesema nchi za Oman imekubali kuisaidia Zanzibar kiuchumi na kuwachukua vijana wa Zanzibar kwenda kufanya kazi nchini Oman kwa mikataba maalum.

Malim Seif alikuwa nje ya nchi kwa muda wa wiki saba ambapo wiki nne alizitumia kuzitembelea nchi za Uholanzi, Sharjah, Dubai na Oman na wiki tatu za mwisho alifanyiwa matibabu ya upasuwaji wa goti nchini India

WAISLAMU WANDAMANA DAR KUPINGA UVAMIZI WA KIJESHI LIBYA

Waislamu mjini Dar es Salaam wamefanya maandamano ya amani kupinga mashambulizi ya nchi za magharibi nchini Libya.

Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Shaban bin Simba amesema waislamu wana haki ya kupinga vitendo hivyo kwa vile raia wa Libya wanashambuliwa katika nchi yao.

Nae mwakilishi wa balozi wa nchi ya Libya nchini Tanzania amesema kitendo kinachofanywa na nchi za magharibi sio tu kumshambulia kuiongozi wa nchi hiyo Kanal Mummar Gaddafi bali ni kushambilia misada aliyokuwa akitoa katika nchi za AFrika.

MATIBABU YANGU INDIA YASIWE MJADALA-MALIM SEIF

Malim Seif akifanya mazoezi baada kufanyiwa upasuwaji wa magoti nchini India

Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema suala la kwenda kutibiwa nje ya nchi halina mjadala kwa vile ni wajibu wa wananchi kuwahudumia viongozi wao.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya matibabu yake ya upasuwaji wa goti nchini India mara baada ya kureja nchini amesema viongozi wa serikali wanamkataba wa kuwatumikia wananchi na wananchi nao wanawajibu wa kuwahudumia viongozi wao.

Malim Seif amesema katika wajibu huo ni kuhakikisha viongozi wana afya nzuri zitakazowawezesha kufanya kazi za kuwaletea maendeleo wananchi.

Hata hivyo amesema fedha nyingi zilizotumika katika matibabu yake haoni dhambi kutumia dola elfu moja huku zikiingia zaidi ya milioni moja

Hata hivyo Malim Seif amesema sio viongozi pekee wanaotibiwa nje ya nchi hata wananchi nao wanapelekwa nje ya nchi kwa ufahdili wa serikali iwapo mgonjwa atakosa huduma zinazohitajika nchini

Malim Seif amesema serikali itahakikisha inatoa huduma bora za matibabu kwa wananchi wake ili kupunguza gharama za kuwasafirisha nje ya nchi.

Katika kampeni zake za kuwania urais wa Zanzibar malim Seif aliahidi yeye na mkewe mama Awena hawatakwenda nje ya nchi kufanyiwa matibabu na badala yake atachokifanya ni kuimarisha huduma hizo.

DAKTARI ATAKAEBAINIKA KUTOA SIRI YA MGONJWA ATAKIONA

Hospitali kuu ya Mnazi Mmmoja Zanzibar

Wizara ya afya imewatakwa wananchi wanaofichuliwa siri zao na madakatari kuwasilisha ushahidi wao ili wafanyakazi hao wachukuliwe hatua za nidhamu.

Taarifa hiyo ya wizara imekuja huku kukiwa na madai baadhi ya wananchi wanashindwa kupima virusi vya ukimwi kwa kuhofia kutolewa siri zao na madaktari endapo watagundulika kuambukizwa ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa wizara hiyo Juma Duni Haji amesema endapo wananchi watashirikiana na wizara hiyo kwa kutoa ushahidi pale wanapofichuliwa siri zao au kuziwa dawa na vitendo vya rushwa.

Amesema hivi karibuni walimkamata mfanyakazi mmoja wa hospitali ya Mnazi mmoja aliedaiwa kuuza dawa baada ya mwananchi alieuziwa dawa hizo kukubali kutoa ushahidi.

Hivyo waziri Duni amewataka wananchi wanaofanyiwa vitendo hivyo kuwasilisha ushahidi wao kunakohusika badala ya kubaki kunungunika