Malim Seif Sharif Hamad

Makamu  wa kwanza wa rais Maalim Seif Sharif Hamad amefanyiwa upasuaji wa goti nchini India katika hospitali ya Apolo Hyderabad jimbo la Andrapradesh imeelezwa.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wasaidizi wake wa karibu wameleza kwamba Maalim Seif anaendelea vyema na matibabu yake na hali yake bado inaendelea ambapo hivi sasa anafanyiwa mazoezi ili goti lake lirudi katika hali yake ya kawaida.

 

Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari  iliyotiwa saini na naibu katibu wa makamu wa kwanza wa rais, Issa Kheri Hussein amesema kwamba Maalim Seif anaendelea kupata matibabu kabla ya kurudi nyumbani baada ya hali yake kutengemaa.

 

Maalim Seif alikuwa katika ziara wiki iliyopita ambapo kwa mujibu wa barua ya ratiba yake ya safari iieleza kwamba mwisho wa safari zake za kiserikali aitapita nchini India kwa uchunguzi wa kiafya.

 

Alikuwa safarini kuanzia Febuari 7 mwaka huu ambapo safari yake ilianzia Uholanzi kwa kushiriki mkutano wa kutimiza miaka ishirini wa kuanzishwa kwa jumuiya ya mataifa ya watu wasio na uwakilishi katika umoja wa mataifa (UNPO) na kuwasilisha mada juu ya maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar .

 

Akiwa Uholanzi pia alifanya mazungumzo na ujumbe wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo juu ya mashirikiano bana ya Tanzania na Uholanzi pia alitembelea  nchini Dubai ambapo pamoja na mambo mengine alikutana na wazanzibari wanaoishi nchi humo na kutembelea maeneo mbali mbali ya kiuchumi.  .

 

Katika ziara hiyo alifuatana na waziri wa fedha,chumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee, waziri wa biashara, viwanda na masoko, Nassor Mazrui, waziri wa kazi, uwekezaji wananchi kiuchumi na ushirika, Haroun Ali Suleiman pamoja na katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa kwanza wa rais, Dk Omar Dadi Shajak.

 

Advertisements