Kampuni ya Zantel inayotarajia kutumia mkonga wa mawasiliano wa taifa baada ya kufikishwa Zanzibar

Serikali ya China imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 21 zinazotarajiwa kutumika katika ujenzi wa mkongo wa taifa upande wa Zanzibar.

Mkataba wa mkopo huo umetiwa saini mbele ya rais Jakaya Kikwete ikulu mjini Dar es Salaam na katibu mkuu wizara ya fedha Ramadhan Kija kwa niaba ya Tanzania na Ge Pein kwa niaba  ya serikali ya China.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo huo, utalipwa ndani ya miaka 20 kutoka sasa.

Mkopo huo umetolewa baada ya kukamilika na kuanza kutumika kwa mkongo huo upande wa Tanzania bara kuliko rahisisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

Advertisements