Majenereta ya Shirika la Umeme Zanzibar ZECO

Kisiwa cha Unguja kinataajia kuanza mgao wa umeme kuanzia leo kutokana na ukosefu wa mafuta ya kuendeshea majenereta yanayozalisha umeme wa akiba.

Afisa uhusiano wa shirika hilo Salum Abdalla Hassan amesema mgao huo utaanzia saa 1.00 usiku hadi saa tano kasorobo za usiku ambapo kila zoni itakosa umeme kwa muda wa saa moja na robo.

Amesema shirika hilo limekuwa likiwasha majenereta kila siku kwa muda wa saa tano kukabiliana na ongezeko la matumizi ya umeme inapofikia nyakati za usiku.

Amesema kutokana na ukosefu wa mafuta shirika hilo litaendelea na mgao hadi pale hali itakapokuwa nzuri na kuweza kumudu kugharamia ununuzi wa mafuta hao

Hata hivyo mgao huo hautayahusu maeneo ya Mji mkongwe kutokana na kuwepo hospital kuu ya Mnazi mmoja.

Advertisements