wafanyakazi wa zantel

Kampuni ya simu za mikononi Zanzibar, Zantel imeanza kulalamikia kushuka kwa mapato kaye kutokana na kile ilichokiita vita vya bei vya kuendesha huduma hiyo ya mawasiliano.

Akizungumza na kamati ya mwasiliano na ujenzi ya baraza la wawakilishi mkurugenzi wa fedha wa Zantel Abdul Wahid Talib amesema hali hiyo imechangia kupungua kwa mapato ya serikali yanayochangiwa na kampuni hiyo kila mwaka.

Amedai ushindani wa bei unaofanywa na kampuni za simu hivi sasa sio ushindani wa kibiashara bali kutaka kufilisi kampuni zinazoendesha huduma za simu za mikononi.

Kutokana na hali hiyo mkurugenzi huyo ameiomba serikali kuangaliwa uwezekano wa kisheria kudhibiti kampuni alizodai zinachafua uendeshaji wa biashara ya mawaslianao ya simu.

Wakati huo huo Spika wa barazala wawakilishi Pandu Ameir Kificho ameiomba kampuni ya Zantel kuangalia uwezekano wa kuwakopesha wajumbe wa baraza hilo Lapt Top ili ziwasaidie kupata mawasiliano.

Spika Kificho ametoa ombi hilo mara baada ya kupokea vifaa vya mawasiliano vya Internet vilivyotolewa msaada na kampuni ya Zantel kwa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo afisa wa uhusiano wa Zantel Charles Juta amesema vifaa hivyo vitawasaidia Wajumbe wa baraza hilo kupata taarifa na kuJIelimisha katika utendaji wa kazi zao.

Amesema kampuni ya Zantel imeamua kutoa msaada huo ili kugawana faida na wateja wake ambapo wajumbe wa baraza la wawakilishi ni miongoni mwa viongozi wanaowakilsha wananchi hao.

Advertisements