Chuo kikuu cha taifa Zanzibar SUZA kinatarajia kumtawadha rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein kuwa mkuu wa chuo hicho Jumanne ijayo.

Taarifa ya chuo hicho iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema Dr. Shein atakuwa mkuu wa chuo hicho baada ya rais mstaafu Dr. Amani Abeid Karume kumaliza muda wake wa mihula miwili.

Sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 29 mwezi huu katika viwanja vya chuo hicho Vuga zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na kimataifa pamoja na wananchi.

Advertisements