Eneo la Mpigaduri Zanzibar linalotarajiwa kujengwa bandari ya mizigo

Makamo wa kwanza wa rais wa Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar inatarajia kupata ufadhili wa ujenzi wa bandari huru na kuendeleza maeneo ya biashara kutoka nchi za falme za kiarabu.

Akizungumza na wandishi wa habari mara baada ya kurejea akitokea nchi za Falme za kiarabu na Oholanzi amesema Dubai na Sharjah zimekubali kusaidia Zanzibar katika ujenzi wa mpya bandari na maeneo ya biashara huru.

Malim Seif amesema amezungumza na wafanyabiashara wakubwa wa nchi hizo pia kuangalia uwezekano wa kuwekeza Zanzibar ili kuisaidia kuimarisha uchumi wake.

Amesema serikali itafuatilia ahadi zilizotolewa na nchi hizo za kuisaidia Zanzibar kiuchumi ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo inafanikiwa

Amesema kwa upande wa serikali itahakikisha inaweka miundo mbinu itakayosaidia kuweka mazingira mazuri ya miradi ya kiuchumi, huku ikijua miradi hiyo inahitaji fedha nyingi.

Aidha Malim Seif amesema nchi za Oman imekubali kuisaidia Zanzibar kiuchumi na kuwachukua vijana wa Zanzibar kwenda kufanya kazi nchini Oman kwa mikataba maalum.

Malim Seif alikuwa nje ya nchi kwa muda wa wiki saba ambapo wiki nne alizitumia kuzitembelea nchi za Uholanzi, Sharjah, Dubai na Oman na wiki tatu za mwisho alifanyiwa matibabu ya upasuwaji wa goti nchini India

Advertisements