Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profisa Ibrahim Lipumba amesema serikali ya Mapinduzi Zanziar inahitaji muda zaidi wa kupunguza gharama za maisha kwa wananchi.

Amesema katika kipindi cha miezi minne bado ni kidogo kupima uwezo wa serikali wa kukabiliana na gharama za maisha na kuwataka wananchi kuvuta subra.

Hata hivyo Profisa Lipumba amewataka wananchi wasichoke kuihoji serikali yao juu ya azma yake ya kuleta maisha bora kwa kila mzanzibari.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Kibandamaiti amesema Zanzibar inafursa nyingi za kuendeleza uchumi ikiwemo shughuli za bandari, kilimo na sekta ya biashara na utalii

Prifisa Lipumba amesema anaimani serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar inaweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kutatua tatizo la ajira kwa vijana, hivyo amewataka wananchi kuendelea kuinga mkono.

Nae mwenyekiti wa chama cha NCCR-MAGEUZI taifa James Mbatia akizungumza katika mkutano huo amesema mabadiliko ya katiba yaliofanywa Zanzibar na kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa yameleta changamoto kwa Tanzania.

Amesema maadiliko hayo ambayo pia yamegusa katiba ya jamhuri ya muungano Tanzania yamechochea kwa kiasi kikubwa kutaka kuandikwa kwa katiba mpya.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwashukuru wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa kuinga mkono wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana.

Advertisements