Archive for April, 2011

VIWANJA VYA NDEGE ZANZIBAR KUFANYIWA MATENGENEZO NA UTURUKI

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetiliana saini makubaliano ya maelewano na Makampuni matatu makubwa ya Uturuki ambayo yatashughulikia ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Unguja na Pemba. 

 

Makubaliano hayo yaliyiwa saini jana katika Hoteli ya Sheraton mjin Ankara Uturuki, ambapo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zazibar iliwakilishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Mhe. Omar Yussuf Mzee.

 

Akizungumza kabla ya kutiwa saini makubaliano hayo, Mhe. Mzee alsema kuwa mradi huo ambao umekisiwa kuharimu kiasi cha Dola za Kimarekani miliono 40, utahusisha matengenezo makubwa katika uwanja wa ndege wakimaifa wa Zanzibar unaotumika hivi sasa kwa ujenzi wa jengo la abiria.

 

Aidha, alisema kuwa kwa upande wa uwanja wa ndege wa Pemba, Kampuni hizo zitaujenga uwanja huo pamoja na kutiwa taa ili kuwezesha ndege kuweza kutua usiku na mchana pamoja na matengenezo mengine.

 

Mhe. Mzee alisema kuwa serikali inaendelea na hatua kukamilisha mkataba kwa ajili ya mradi huo ili ikiwezekana utekelezaji wake uanze katika mwaka ujao wa fedha.

 

Nae mwakilishi wa Makampuni hayo ya YDA-ORIZZONTE-SARAYLI (YDA –ORSA) Bwana Huseyin Arslawa alisema kuwa hatua hiyo ni mwanzo katika utekelezaji wa miradi mengine inayokusudiwa kuekezwa na makampuni hayo kwa hapa Zazbar.

 

Alisemasambamba na utekelezaji wa mradi huo Kampuni hiyo itajenga hoteli ya kisasa kisiwani Pemba ambayo inatarajiwa kuanza kazi rasmi mara tu baada yakukamilika kwa ujenzi wa uwanja huo wa ndege.

 

Pamoja na hayo alisema kuwa Uturuki imemeamua kwa dhati kuelekeza nguvu zake  za uwekezaji katika nchi za Afrika hasa katika maeneo ambayo amani na utulivu vimetawala ikiwemo Zanzibar.

 

Hatua hiyo imekuja kufuatia ziara ya Rais wa Zanzibr na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ambaye yupo nchini Uturuki kwa ziara ya mwaliko wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Abdallah Gul.

 

MATOKEO YA KIDATU CHA SITA 2011

MATOKEO HAYA NI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA BARAZA LA MITIHANI TANZANIA

THE NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

KUANGALIA MATOKEO BONYENZA LINKS ZA CHINI.

f LINK 1: MATOKEO KIDATO CHA SITA

f LINK 2: MATOKEO KIDATO CHA SITA

f LINK 3: MATOKEO KIDATO CHA SITA

KIKWETE ATOWA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 3060

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Misho Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa Elfu tatu na 60 katika kusherehekea miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya ndani Shamsi Vuai Nahodha waliopata msamaha huo ni wafungwa wenye maradhi sugu kama ukimwi, kifua kikuu na saratani.

Wengine ni wazee wenye umri wa miaka sabini, wafungwa wa kike waliofungwa gerezani wakiwa na mimba na wale walioingia na watoto wachanga na waliokuwa wanatumikia vifungo vya miaka mitano ambayo hadi leo watakuwa wametumikia robo ya vifungo vyao.

WANAOSEMA HAWATAKI MUUNGANO WANAYO HAKI-SITTA

Samuel Sitta

Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta amesema baadhi ya wananchi wasiotaka muungano wana haki ya kutoa maoni yao hayo, lakini wazingatie muungano huo umekuwa na faida kwa pande zote mbili.

Akizungumza na Zenji Fm radio kuhusu mafanikio ya miaka 47 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, amesema baadhi ya wananchi wamekuwa na jazba wanapojadili masuala ya muungano.

Waziri Sita amesema muungano umekuwa na faida kubwa kuliko hasara na watanzania wanaendelea kuishi pamoja, kufahamiana , kuwepo kwa fursa za kiuchumi akiutaja mradi wa TASAF.

Amesema mradi huo ulikuwa ni wa Tanganyika pekee, lakini umeelekezwa kutatua matatizo ya vijijini kwa upande wa Zanzibar

Akizungumzia ugawaji wa pato la simian 4.5 kwa Zanzibar amesema suala hilo halikufikiwa na upande mmoja, lakini wataalamu wamezingatia vigezo kama vile idadi ya watu na umsikini.

Hata hivyo amesema baadhi ya watanganyika nao pia wanalalamika na kusema Zanzibar inapendelewa ndani ya muungano.

Waziri Sita amefahamisha baadhi ya wazanzibari hawatembei upande wa pili kusikikia malalamiko hayo

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa na viongozi wa nchi hizo mbili Marehemu Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1964.

UINGEREZA YAHIDI KUISAIDIA ZANZIBAR

UINGEREZA imeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wake  uliopo kati yake na Zanzibar na kuahidi kuendelea kuunga mkono uimarishaji  miradi ya maendeleo ukiwemo mpango wa kusomesha lugha ya kiengereza kwa skuli za Zanzibar.

 

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Dianne Conner, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Ikulu mjini Zanzibar.

 

Katika  mazungumzo yake, Balozi Corner alisema kuwa  Uingereza inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Zanzibar ambao ni wa kihistoria na kuahidi kuuimarisha zaidi hasa katika kuunga mkono miradi ya maendeleo.

 

Alisema kuwa nchi yake itaendelea kutoa ushirikiano na misaada yake kwa skuli za Zanzibar kwa lengo la kuimarisha lugha ya kiengereza.

 

Balozi Corner alisema kuwa Uingereza itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania ikiwemo Zanzibar kutokana na nchi hiyo kuwa mdau mkubwa wa Tanzania.

 

Alisema kuwa katika juhudi za kuimarisha uhusiano na ushirikiano ulipo kati yake na Tanzania ikiwemo Zanzibar nchi yake  pia, imeahidi kuendelea kuiunga mkono bajeti ya  Tanzania.

 

Akizungumzia kuhusu sekta ya utalii, Balozi Corner alipongeza na hatua zinazochukuliwa na serikali  katika kuimarisha sekta hiyo na kuahidi kuitangaza Zanzibar  nchini mwake ili watalii wengi kutoka nchi hiyo waweze kuitembelea Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

 

Katika mazungumzo hayo pia,  Balaozi Corner aliendelea kutoa pongezi kwa mara nyengine tena kwa Dk. Shein pamoja na wananchi wa Zanzibar kwa kufanya uchaguzi uliokuwa wa amani na utulivu mkubwa.

 

Pamoja na hayo, Balozi Corner alifurahishwa na mipango ya maendeleo ya Mji Mkongwe iliyowekwa na serikali pamoja na historia ya mji huo na kuahidi kuunga mkono juhudi zote za kuimarisha mji huo.

 

Balozi huyo pia, alieleza haja ya kuendelea kutunzwa na kutangazwa zaidi kwa Mji Mkongwe wa Zanzibar  kutokana na historia na haiba yake sanjari na mambo mengine  yaliomo ndani yake.

 

Nae Dk. Shein kwa upande wake alitoa salamu zake za shukurani kwa Balozi huyo pamoja na uongozi wa nchi hiyo kwa juhudi zake za kuendeleza uhusiano na ushirikiano wake wa kihistoria na Zanzibar.

 

Alieleza kuwa Zanzibar inatambua kuwa uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Uingereza ni wa kihistoria na ndio maana inaona haja  ya kuendelea kuuimarisha zaidi.

 

Aidha, Dk. Shein alitoa pongezi kwa nchi ya Uingereza kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania ikiwemo Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo sanjari na hatua yake ya kuendelea kuisaidia bajeti ya Tanzania.

 

Dk. Shein alimueleza Balozi Corner kuwa juhudi kubwa zimekuwa zikichukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuimarisha miradi yake ya maendeleo ambapo hatua ya nchi hiyo kuendelea kuiunga mkono Zanzibar kutasukuma na kuendeleza mbele juhudi hizo.

 

Alisema kuwa  serikali anayoingoza imekuwa ikifanya kazi kwa pamoja na mashirikiano makubwa kwa kutambua kuwa mafanikio yanayopatikana ni kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote.

 

Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein aliendelea kusisitiza kuwa amani na utulivu iliyopo Zanzibar ni njia moja wapo ya kuzidisha na kuimarisha maendeleo yaliofikiwa.

 

Kwa upande wa Mji Mkongwe wa Zanzibar, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuuhifadhi na kuulinda mji huo kutokana na umuhimu wake mkubwa.

 

Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni kuendeleza juhudi za makusudi katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula na uhifadhi wake na ndio maana serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha sekta ya kilimo na sekta nyenginezo hapa nchini.

 

Sambamba na hayo, Dk. Shein alisisistiza kuwa serikali imeweka vipaumbele  katika sekta zote za maendeleo hapa Zanzibar kwa kutambua umuhimu wake mkubwa katika maendeleo ya nchi na wananchi wake.

ZANZIBAR YAJIVUNIA AMANI YA UWEKEZAJI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekii wa Barza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa kuwepo kwa amani na utulivu Zanzibar ni miongoni mwa vivutio vikubwa vya uwekezaji katika sekta mbali mbali za maendeleo.

 Rais Dk. Shein aliyasema hayo leo katika Mkutano wa Uwekezaji Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Mlimani mjini Dar-es-Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi za Afrika Mashariki pamoja na wawekezaji mbalimbali.

 Akitoa maelezo yake mafupi katika mkutano huo ambao Mwenyekiti wa mkutano huo ni Rais wa Burundi Mhe Piere Nkurunziza, Dk. Shein alisema kuwa kuwepo kwa amani na utulivu Zanzibar ni hatua moja wapo ya kivutio kikubwa cha uwekezaji.

 Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi anzibar imekuwa ikichukua juhudi za makusudi katika kuhakikisha sekta ya uwekezaji inapata mafaniki makubwa kwa kuiwekea mazingira mazuri.

 

Alizema kuwa miongoni mwa mazingira hayo ni pamoja na kuweka Wizara husika inayoshughulikia sekta nzima ya uwekezaji pamoja na kuwepo kwa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA).

 Aidha, Dk. Shein alisema kuwa kwa upande wa Zanzibar vipaumbele vyote vya sekta ya maendeleo vinahitajika ikiwa ni pamoja na elimu, afya, miundombinu, maji, kilimo na vyenginevyo.

 Katika maelezo yake Dk. Shein alieleza kuwa mbali na hatua hizo zilizochukuliwa pia, suala zima la Utawala Bora nalo limeweza kuchukua nafasi nzuri kwa upande wa Zanzibar hatua ambayo imeweza kuchangia kuwepo kwa mazingira bora ya uwekezaji.

 Pamoja na hayo, Dk. Shein alisema kuwa hatua za makusudi pia, zinachukuliwa katika kuhakikisha wawekezaji wa ndani nao wanapewa kipaumbeleza zaidi ili waweze kuekez nchini mwao.

 Aidha, Dk. Shein alisema kuwa kwa vile Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeweza kupata mafanikio makubwa sanjari na mashirikiao ya pamoja ya taasisi za uwekezaji katika suala zima la kuiimarisha sekta hiyo.

 

Mapema akifungua mkutano huo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, alieleza kuwa Tanzania imejiandaa na inaendelea kujiandaa vilivyo katika kuimarisha sekta ya uwekezaji hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuiimarisha bandari kuu ya Dar-es-Salam na barabara kuu ziendazo katika nchi zote jirani na Tanzania kwa kuhakikisha zinajengwa katika kiwago cha lami pamoja na kuweka Sera madhubuti za uwekezaji.

 Alisema kuwa Tanzania ina maeneo mengi ya uwekezaji hivyo aliwata wawekezaji kutoka sehemu mbali mbali duniani kuja kuekeza Tanzania huku juhudi za makusudi zikiendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha mazingira mazuri yanawekwa.

 Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunzinza alisema kuwa  Jumuiya hiyo imepata mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake  ikiwa ni pamoja a kuendeleza ushirikino na uhusiano mwema kati ya wanachama wake sanjari na kujijengea mustakabali mzuri kiuchumi.

 Mwenyekiti huyo aliwapongeza wawekezaji wazalendo walioko katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kufanya kazi kubwa na nzuri katika lengo zima la kukuza uchumi.

 Pamoja na hayo, Mwenyekiti huyo alisisitiza haja ya Mabenki kubadilika na kuweza kuwaunga mkono wawekezaji hasa wale wazalendo.

 Katika meza ya duara ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Mwenyekiti kwa upande wa Tanzania, Tanzania iliweza kutangaza maeneo yake mbali mbali ya uwekezaji ambapo sekta ya kilimo kwa upande wa Tanzania Baraza ilielezewa kwa mapaa zaidi  pamoja na ile ya Utalii kwa Zanzibar.

 Kwa upande wa Zanzibar akitoa maelezo yake juu ya mkutano huo, Mkurugenzi wa ZIPA Salum Nassor alisema kuwa Zanzibar ina maeneo mengi ya uwekezaji hasa katika sekta ya utalii, uvuvi na kilimo hasa cha mboga mboga kutokana na uhaba wa ardhi yake.

 Alisema kuwa Zanzibar ni visiwa vilivyozungukwa na bahari hivyo uwekezaji katika sekta ya uvuvi nayo inaweza kuchukuwa nafasi kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwepo kwa kiwango kkuwa cha samaki katika mzunguko wa visiwa hivyo.

 Alisema kuwa juhudi pia, zinachukulwia katika kuhakikisha zao la karafuu nalo linapewa kipaumbele katika kuhakikisha nalo linawekwa katika jumla ya uwekezaji kwenye sekta ya kilimo kutokana na umuhimu wake mkubwa.

 Sambamba na hayo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa serikali tayari imeweka maeneo ya vitega uchumi kwa upande wa Unguja na Pemba ambayo yako katika hali nzuri na mazingira bora kwa uwekezaji.

 Katika mkutano huo wa siku mbili viongozi mbali mbali Kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walihudhuria akiwemo Rais wa Burundi ambaye ndiye Mwenyekiti wa EAC kwa sasa Rais Pierre Nkurunzinza, Rais wa Kenya, Mwai Kibaki, Rais wa UgandaYower Museven, Waziri Mkuu wa Rwanda Bernad Makuza na viongozi wengineo

MTANGAZAJI MKONGWE ZANZIBAR JOSEPH ASAMA AMEFARIKI DUNIA

Mtangazaji mkongwe Zanzibar, Joseph Caitan Asama(79) amefariki dunia jana mchana huko nyumbani kwake Mbweni Zanzibar.

Marehemu Asama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu na alizidiwa jana mchana wakati akiwa katika matayarisho ya kwenda Hospitali Mnazi Mmoja kwa matibabu na hatimaye kufariki dunia.

Misa ya marehemu Joseph Caitan Asama itafanyika kesho mchana  katika Kanisa la Anglikana  Mbweni nje kidogo ya Manispaa ya Zanzibar na kutarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Unguja saa 9:00 Alasiri.

 

Viongozi mbalimbali wa juu wa Serikali pamoja na wananchi wanatarajiwa kuhudhuria katika mazishi ya mtangazaji huyo mkongwe wa Sauti ya Tanzania Zanzibar, marehemu Joseph Asama.

Joseph Asama, alizaliwa tarehe 12/07/1932 Kisima Majongoo Unguja na   ni miongoni mwa  wa watangazaji wa mwanzo katika Tasnia ya Utangazaji  kwa wakati huo Visiwani Zanzibar. Alianza kazi katika miaka ya mwishoni mwa hamsini katika Idara ya Habari na Utangazaji akiwa katika sehemu ya Utangazaji ya Sauti ya Unguja kabla ya kuwa Sauti ya Tanzania Zanzibar.

Ukiacha uzoefu katika utangazaji, marehemu Joseph Asama alikuwa  Mkuu wa vipindi wa STZ, Mwandishi wa Habari  wa Rais wa Zanzibar na Makamu wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi,Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Utangazaji pamoja na kuwa Afisa Uhusiano wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar.

Marehemu Joseph Asama, ameacha kizuka mmoja na watoto wawili.