Wafuasi wa CCM na CUF wakiwa katika maadhimisho ya miaka 47 ya mapinduzi Zanzibar yaliofanyika uwanja wa Amani, mjini Zanzibar.

Wafuasi wa vyama vya siasa Zanzibar wamesema ushirikiano wao katika shughuli za maendeleo na kijamii umekuwa mkubwa ukilinganishwa na kipindi cha nyuma kabla ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa.

Wakizungunza na waandishi wa habari wanaoshiriki mafunzo yanayoendeshwa na taasisi ya Seach for Common Ground wamesema bado kuna asilimia ndogo ya wananchi wasiopenda ushirikiano kwa maslahi binafsi

Wamesema ushirikiano huo uliotokana na maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa kati ya aliyekuwa rais wa Zanzibar dr Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF maalim Seif Sharrif Hamadi baada ya kuonekana Zanzibar inaelekea mahala pabaya.

Hivyo wananchi hao wameshauri kuongeza ushirikiano uliopo ili kuendeleza amani na utulivu nchini

Nao viongozi wa vyama vya siasa wamesema ushirikiano huo unaweza kutoweka iwapo kutakuwa na hali ya kutoaminiana na inaweza kuwa chanzo cha mgawanyiko kwa wananchi.

Mkurugenzi wa haki za binadamu, habari na uenezi wa CUF Salim Bimani amesema viongozi wanaendelea kuwa wamoja bila ya kujali sera na itikadi za vyama vyao vya kisiasa

Advertisements