Mwanaharakati wa CHADEMA Ali Omar

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kinatarajia kufanya maandamano ya amani kupinga muswada wa sheria wa kuanzisha tume ya kukusanya maoni ya wananchi ya kuandikwa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano Tanzania.

Akizungumza na Zenji Fm radio pembezoni mwa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Kibandamaiti juzi, mwanaharakati wa CHADEMA Ali Omar amedai Zanzibar haipewi mambo ya msingi ya kujadili muungano.

Amesema wiki hii wanatarajia kuwasilisha barua rasmi ya kuomba ruhusa ya kufanya maandamano hayo kwa jeshi la polisi Zanzibar.

Omar amesema maandalizi ya maandamano hayo yanaendelea vizuri, huku akivitaja vyama vya TADEA, NCCR-MAGEUZI na AFP vikitarajia kushiriki katika maandamano hayo

Jumapili iliyopita chama hicho kimechoma moto hadharani rasimu ya muswada huo kwa madai ya kutaka kumezwa mamlaka ya Zanzibar

Advertisements