Salim Bimani, Naibu Mkurugenzi wa Haki

Chama cha wananchi CUF kimelalamikia kitendo cha kuhusishwa na matukio ya ghasia zilizotokea katika upokeaji wa maoni ya wananchi ya undwaji wa kamati ya kukusanya maoni uliofanyika hapa Zanzibar.

Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari imesema habari hizo zilizoandikwa na gazeti moja linalochapishwa mjini Dar es salaam sio za kweli na lengo lake ni kuwapotosha wananchi.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na mkurugenzi wa haki za binadamu na uwenezi CUF Salim Biman imedai chama hicho hakitaridhia kudhalilishwa na kudhoofishwa mbele ya wananchi.

Hivyo kimetaka vyombo vya habari na mwandishi wake walioandika habari hizo kuomba radhi la sivyo kitachukua hatua za kisheria

Advertisements