Wanawake nchini wameshauriwa kuzungumzia zaidi masuala ya maendeleo kwa kutumia raslimali ziliopo kufuatia kufikiwa kwa maridhiano ya kisiasa.

Wito huo umetolewa na afisa wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA, Zanzibar Mzuri Issa alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari walioko kwenye mafunzo yanayoendeshwa na taasisi ya Search for Common Ground kuelezea maendeleo ya wanawake baada ya maridhiano ya kisiasa.

Amesema licha ya kuwepo maridhiano ya kisiasa, lakini ni vyema kwa wanawake kuangalia mambo yanayoweza kuwaendeleza kiuchumi na kijamii badala ya kushughulikia siasa pekee.

Mzuri amesema TAMWA kupitia mradi wa kuwaendeleza wanawake wa Zanzibar kiuchumi WEZA inaendelea kuwahamasisha wanawake kuitumia siasa kwa kutafuta mbinu za kuingia kwenye maendeleo yao

Nao wanavikundi vya WEZA wakizungumza juu ya maendeleo yao baada ya maridhiano wamesema wanaendelea kushirikiana hasa katika uanzishwaji wa vikundi vya uzalishaji bila ya kujali tofauti zao za kisiasa.

Wamesema mbali na kuwepo maridhiano ya kisiasa, lakini mradi wa WEZA umewasaidia kuwaunganisha wanawake kuwa wamoja katika masuala ya maendeleo, kijamii na kutetea haki zao za msingi.

 

Advertisements