Watu watano wamekufa na wengine 45 kujeruhiwa baada kuungua moto wakati wakijaribu  kuchota mafuta  kwenye lori lililopata ajali kabla ya petrol kulipuka mkoani Singida.

Kamanda wa polisi  mkoa wa Singida Celina Kaluba amesema tukio hilo limetokea jana  usiku katika eneo la mzunguko- Mjini Manyoni barabara kuu ya Singida-Dodoma.

Amesema  mapema majira ya saa 12 jioni  lori la mafuta  aina ya Scania  lilipata ajali  katika eneo  hilo  baada ya kugonga kichwa cha  Trein kilichokuwa kinatoka kituo cha Aghondi kwenda Manyoni  Mjini.

Amesema baada  ya ajali  hiyo  polisi waliweka askari kwenye eneo la tukio kulinda  lori hilo lililokuwa linasafirisha zaidi ya lita elfu arobain za mafuta  ya petroli toka  Dar-es-Salaamu kwenda Mwanza.

Kamanda Kaluba amesema majira ya saa 2 usiku  wananchi walijaribu kuchota mafuta  kutoka kwenye sehemu  iliyopasuka Lori hilo lililipuka na kusababisha vifo vya watu  wanne papo hapo na wengine 45 kujeruhiwa wakiwemo  askari  polisi 15

Miili ya watu wengine wawili  haijatambuliwa kutokana na kuungua  vibaya kwa moto kiasi cha  kushindwa kufahamika.

Mganga  wa wilaya ya Manyoni  Dk Antipas Swai anasema hali  za majeruhi wengi ni mbaya  kutokana na kuungua  sehemu za tumbo na mgongoni

Advertisements