Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi wameishauri serikali ya mapinduzi Zanzibar kuishawishi serikali ya Jamhuri ya muungano Tanzania kutambua uraia wa nchi mbili ili waweze kusaidia maendeleo ya nchi yao.

Wakizungumza na wandishi wa habari walioko kwenye mafunzo yanayoendeshwa na taasisi ya Search for Common Ground wamesema hakuna mipango maalum inayowaunganisha wazanzibari wanaoishi nje kusaidia nchi yao.

Mmoja wa Wanzibari hao Ramadhan Omar Juma amesema watu wenye asili ya Zanzibar wamewekeza katika nchi tofauti duniani wakiwa na uraia wa nchi nyingine, lakini wanakosa fursa za kuja kuwekeza nchini kama wazalendo kutokana na kubadilisha uraia wao.

Hivyo ameishauri serikali kutoa upendeleo maalum kwa wawekezaji hao kuja kuwekeza Zanzibar kama wazalendo badala ya kuwakumbatia wawekezaji wa kigeni

         Nae Makamo wa kwanza wa rais Malim Seif Sharif Hamad akizungumza na wandishi wa habari baada ya kurejea ziara ya kikazi nje ya nchi amesema serikali imeanza kuwatambua wazanzibari wanaoishi nje ya nchi ili kusaidia maendeleo ya nchi yao.

Amesema katika ziara yake nchini Oman alizungumza na watanzania ambao waliunga mkono suala la kuchangia nchi yao na wanachotaka ni utekelezaji.

Malim Seif amesema serikali kupitia Idara ya uratibu wa wanzibari wanaoishi nchi za nje inafanya utaratibu wa kuwajuwa nchi wanazoishi, taaluma zao na uwezo wao wa kuichangia Zanzibar

Advertisements