Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Rahma Mshangama,aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa jamii,maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto,aliyezikwa jana katika makaburi ya mwanakwerekwe mjini Unguja.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mahhemd Shein leo ameongoza maziko ya aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya ustawi wa jamii maendeleo ya wanawake na watoto Rahma Mohammed Mshangama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idra ya habari maelezo Zanzibar marehemu alikuwa na umri wa miaka 50 na amezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe baada ya Sala ya Ijumaa.

Wakati wa uhai wake marehemu alifikia kiwango cha elimu ya shahada ya pili katika uzalishaji wa wanyama alioipata katika kikuu cha Reading nchini Uingereza na shahada ya kwanza katika fani ya kilimo katika chuo kikuu cha Sokoine mjini Morogoro.

Katika uhai wake marehemu aliwahi kushika nafasi mbali mbali katika serikali ya mapinduzi Zanzibar ikiwemo wizara ya ustawi wa jamii, maeandeleo ya wanawake na watoto na hadi kufa kwake.

Nafasi nyengine ni pamoja na katibu mkuu wa wizara ya kilimo, maliasili, mazingira na ushirika, katibu mkuu wa wizara ya nchi wanawake na watoto, mkuu wa kitengo cha mifugo, mkuu wa kitengo cha wakulima katika katika kamisheni ya kilimo na mifugo na afisa msaidizi mipango katika shirika la chakula duniani WFP.

Mungu ailaze mahala pema Peponi roho ya marehemu AMEN

Advertisements