Kiongozi (Amiri) wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Mselem Bin Ali akizungumza katika mhadhara ulioandaliwa na jumuiya hiyo katika viwanja wa Skuli ya Lumumba Mjini Unguja ( Picha kwa hisani ya Zanzibar Yetu Blog)

Jumuiya ya Uamsho na mihadhara ya kislamu imetaka Zanzibar kurejeshewa kiti chake katika umoja wa mataifa kwa vile ni nchi huru.

Akizungumza katika mhadhara wa kislamu uliofanyika viwanja vya Lumumba Amir wa jumuiya hiyo Sheikh Mselem Ali amesema Zanzibar ni nchi kamili na ilikuwa na kiti katika umoja wa matafia.

Amesema Zanzibar iliungana na Tanganyika kama nchi kamili ikiwa na serikali yake na katiba, hivyo wakati umefika sasa wa kurejeshewa kiti hicho

Aidha Sheikh Mselem amewataka waislamu kuungana pamoja na kutoruhusu mwanya wa kuwagawa na kujenga ustarabu wa kutekeleza mambo yao kidiplomasia.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimami Zanzibar Amir Farid Adi amelilalamikia jeshi la polisi kwa kuwanyima wananchi haki ya kikatiba ya kuwasilisha maoni yao kwa njia ya maandamano.

Amesema sababu zilizotolewa na jeshi hilo za kuzuwia maandamano ya waislamu yaliokuwa yafanyike jana hazikuwa na msingi na kuwanyima haki yao ya kikatiba

Advertisements