Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Piuse Msekwa

Makamo mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Piuse Msekwa amesema mageuzi yaliofanywa na uongozi wa juu wa chama hicho hayatoishia katika ngazi ya taifa, na badala yake yataendelea hadi ngazi za mashina.

Akizungumza na wana CCM katika mkutano wa kuwatambulisha viongozi wapya amewataka wanachama kuyaunga mkono mageuzi hayo kwa vile yanalenga kurejesha heshima na imani kwa wananchi.

Amesema kabla ya kufanywa mabadiliko hayo ilionekana wananchama kukatishwa tamaa kutokana na kupungua kwa ushindi wa uras, wabunge na madiwani kwa upande wa Tanania bara

Amesema kazi, kubwa itakayofanywa na sektarieti mpya ya chama cha mapinduzi ni kurekebisha kasoro ziliozoondoa matumaini ya wananchi pamoja na kupambana na ufisadi

Nae naibu katibu mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema uongozi wa chama hicho hautaruhusu kuvuruga umoja na mshikamano katika kukijenga chama hicho

Advertisements