Archive for May, 2011

MWANDISHI WA HABARI ANYANYASWA ZANZIBAR

Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar
(WAHAMAZA)

25 Mei, 2011

Kuh: Kukamatwa Haji Bwegege, TBC

Chama cha Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) kimesikitishwa
na tukio la kukamatwa Mwandishi Haji Bwegege wa Shirika la Utangazji
Tanzania (TBC)  jana Mei 24 wakati akiwa kazini.

Kitendo cha kukamatwa Haji Bwegege kimetokea katika eneo la Makontena
Darajani wakati akifanya kazi yake halali na katika eneo ambalo
halilindwi kisheria.

Mwandishi huyo alikuwa akifuatilia kadhia ya Makontena ambayo kwa
hakika Mahakama Kuu ya Zanzibar tayari imeshatoa amri kuwa Makontena
hayo yaliokuwa yamefungiwa na Manispaa ya Zanzibar yafunguliwe wakati
shauri la kesi iliyo Mahakmani iliyofunguliwa na Wafanyabiashara hao
likisubiri kusiki8lizwa.

Mwandishi alikuwa akifanya wajibu wake kuona kuwa amri ya Mahakama
inatekelzwa katika hali ambayo ni wajibu wa taasisi za Serikali kuwa
mfano wa Utawala Bora, ambapo amri ya Mahakama iliyotolewa Alkhamis
iliypita hadi jana ilikuwa bado haijatekelezwa.

Wana vikosi wanaofanya lindo katika eneo hili hii ni mara ya pili
kunyanyasa waandishi wa habari wanapofika katika eneo hilo , mara ya
kwanza ikiwa ni dhidi ya Mwandishi Munir Zakaria wa Channel Ten.

Jambo hili halikubalika hata kidogo tukijua kuwa Rais wa Zanzibar Dk
Ali Muhammed Shein katika hotuba yake ya kuingia Serikali alisema kuwa
utawala wake utakuwa karibu na vyombo vya habari na utaheshimu uhuru
wa vyombo vya habari.

Haya yakitokea waandishi wa habari wa Zanzibar kwa ujumla hawaridhiki
na namna wanavyowekwa kando na mfumo mzima wa Serikali ya zanzibar na
kwa ujumla ikiwawia vigumu kupata habari, kama alivyotanbahisha Dk
Shein alipozungumza na watendaji wa Serikali baada ya semina elekezi
lakini pia kurudia baada ya ziara yake ya Mkoa Mjini Magharibi.

WAHAMAZA inatoa wito kwa Serikali kuchukua hatua ya kutoa maelekezo
kwa vyombo vya ulinzi vikiwemo Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari na kuwawacha waandishi
wa habari wafanya kazi yao kama mhimili wa nne wa dola.

Pia WAHAMAZA inapenda kutoa wito wa Serikali kujivua gamba katika
suala zima la kutoa habari na kufungua milango kwa wananchi, ambao
hivi sasa miezi sita tokea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa,
hawajui mengi kuhusu Serikali yao na kwa hivyo si waelewa wa
kilichofanyika na kisichoweza kufanyika hadi sasa, lakini zaidi kwa
sababu gani na huku hali yao ya maisha ikiwa ngumu zaidi.

WAHAMAZA inapenda kutoa ahadi kuwa iko tayari kufanya kazi na Serikali
kwa karibu zaidi kwa kuelewa kuwa vyombo vya habari ni kiungo muhimu
baina ya Serikali na wananchi na tunajua kuwa Serikali iliyochaguliwa
na watu haitaki kujitenga na wapiga kura na wananchi.

Katibu wa WAHAMAZA

………………..

Salma Said

WAFANYA BIASHARA WA UINGEREZA KUWEKEZA Z,BAR

Uingereza imeahidi kuimarisha ushirikiano wa  biashara na Zanzibar kwa manufaa ya pande mbili hizo.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Henry Bellingham ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar alipokuwa akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,

Amesema kuwepo serikali ya Umoja wa Kitaifa imesaidia kuleta amani na utulivu jambo ambalo limewafanya wawekezaji na wafanyabiasahara wavutika kuweka vitega uchumi vyao Zanzibar.

Waziri huyo amesema Utalii na Biashara ni miongoni mwa mambo yatakayoekezwa na waekezaji wa Uingereza na kuahidi kuwahamasisha waekezaji na wafanyabiashara wa nchi hiyo waje kuekeza Zanzibar.

Nae Dk. Shein alimueleza waziri huyo Zanzibar imejiandaa kuwakaribisha wawekezaji na imeweka mazingira mazuri.

Aidha, Dk. Shein aliahidi kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Zanzibar na Uinmgereza ili kuleta maendeleo kwa nchi zote mbili.

KESI ZA UBAKAJI DHIDI YA WATOTO KUPATIWA DAWA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi amewataka wanasheria na vyombo vya Dola kuharakisha mchakato wa kesi za ubakaji ili zisichelewe kumalizika.

Makamu wa Pili wa Rais alitoa ushauri huo katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mkono kwa Mkono (One Step Centre) cha hospitali ya Mnazi Mmoja, kinachoshuhulikia kesi za ubakaji.

Alisema suala la kuzimaliza kesi kwa haraka pasi na kubabaishwa wadau wake litajenga imani kwa wananchi juu ya vyombo vyao na kuepusha watu kuchukua sheria mikononi mwao.

Mheshimiwa Balozi Iddi aliwasihi wazazi na walezi kuondokana na tabia ya kuficha kesi za watoto wao wanapopata matatizo ya kubakwa kwa hofu ya aibu na badala yake wakitumiye kituo hicho kwa ukamilifu.

Alieleza kuwa kituo hicho ni muhimu sana kwa kesi za aina hio kwa kuwa kitasaidia kupatikanwa ushahidi wa uhakika tena kwa haraka kuhusu wahalifu wa kesi hizo.

Mapema Meneja wa Shirika la ‘Save the Children’ Bw. Mubarak Maman aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuonesha mfano mzuri wa uwajibikaji wake kwa suala la udhalilishaji wa watoto kwa kuanzisha kituo hicho.

Kwa upande wake Waziri wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto alisema tafiti nyingi zimeonesha kuwa vitendo vya ubakaji vimekuwa vikiongezeka kila mwaka. Hadi sasa zaidi ya matukio 3,116 yameripotiwa kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2006 – 2010.

Kituo hicho kinachojuulikana Mkono kwa Mkono kimejengwa kwa msaada mkubwa kutoka Shirika la Save the Children na kushirikiana na wafadhili wengine kama UNICEF, DANIDA, UNEPA, USAID na FHI

BALOZI IDDI AKEMEA WATENDAJI WA SERIKALI WANAOUZA MAENEO YA WAZI

Balozi Seif Ali Iddi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi amekemea vikali juu ya tabia mbaya ya baadhi ya watendaji wa Serikali ya kukiuka sheria na taratibu za nchi kwa makusudi ili kuwanufaisha baadhi ya wakubwa.

Makamu huyo wa Pili wa Rais aliyasema hayo alipokutana na Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, hapo Ofisini kwake Vuga.

Alisema kuwa ni jambo la aibu linalofanywa na baadhi ya wanaowania uongozi wakati wa uchaguzi na kuwaomba kura wananchi na baadaye kuwanyanganya haki zao.

“Inasikitisha sana na ni jambo la aibu tunavyofanya baadhi yetu ya kuomba kura wakati wa uchaguzi na baada ya kuchaguliwa kuwanyanganya watu haki zao,” alisema Balozi Iddi.

Alieleza kuwa amegundua sehemu za wazi nyingi wanazopewa wakubwa zinatolewa na vibali halali za mamlaka husika wakati watoa vibali hao na wanaopewa wote wanafahamu kuwa ni kinyume cha sheria.

Hivyo amesema Serikali haitavumilia suala hilo, na alitoa mfano wa viwanja vya kwa Mchina ambako alishauri kama patahitajika kujengwa basi bora Serikali yenyewe ijenge Taasisi itayowahudumia jamiii kwa ujumla.

Kabla ya hapo Mwenyeketi wa Kamati hio Mhe. Makame Mshimba Mbarouk pamoja na Naibu wake Mhe. Rashid Seif walieleza kero zao ikiwa ni pamoja na masuala ya ujenzi wa sehemu za wazi na kupuuzwa kwa ripoti zao za kamati na Wizara husika.

Aidha, kuhusu ripoti za Kamati za Baraza kutoshughulikiwa na Wizara husika Mhe. Balozi Iddi alieleza kusikitishwa kwake na jambo hilo na kusema kuwa Kamati ni muhimu sana kwa kusaidia Serikali na kupunguza makero ya wananchi.

Kwa hivyo aliahidi kulifuatilia suala hilo na kuhakikisha ripoti za Kamati za Baraza zinazingatiwa ipasavyo na kufanyiwa kazi.

DR. SHEIN KUIMARISHA KILIMO CHA MPUNGA BONDE LA CHEJU

Zao la mpunga

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameahidi kuimarisha kilimo champunga katika bonde la Cheju kwa kuliwekea miundombinu ya umwagiliaji ili lizalishe mpunga kwa wingi.

        Dk. Shein ametoa ahadi hiyo akizungumza na wakulima wa bonde hilo katika ziara yake ya Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja nakusema serikali itaendelea kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kuwasaidia wakulima.

Amefahamisha kuwa ahadi zote zlizozitoa wakati wa kampeni baadhi yake zimeanza kutekelezwa na zilizokuwa bado zitachukuliwa hatua ili kuona wananchi na hasa wakulima wanafadika.

Dr. Shein amesema serikali itahakikisha inawapatia wakulima mbegu bora, mbolea, maji na utaalamu, hivyo amewataka wasivunjike moyo na kuahidi ndani ya miaka mitano sekta ya kilimo itakuwa na mabadiliko.

Nae Naibu Waziri wa miundombinu, mawasiliano na Uchukuzi Issa Gavu aliwahakikishia wananchi wa Cheju kuwa barabara kutoka Jendele hadi Unguja Ukuu imo katika mradi wa ujenzi wa Bajeti ya mwaka huu.

BOT YAISHAURI SMZ KUBINAFSISHA KARAFUU

Mkulima akianika zao la karafuu

Benki kuu Tanzania tawi la Zanzibar imesema kuwepo kwa soko huria la ununuzi wa zao la karafuu litaongeza bei kwa mkulima na hivyo kuongeza uzalishaji pamoja na kulingiza taifa fedha za kigeni. Meneja msaidizi wa idara ya uchumi wa benki hiyo Lemo Mwimo amesema tafiti zilizofanywa zinaonesha kuwepo kwa soko hilo kutaongeza imarishaji wa mashamba ya karafuu na kupunguza biashara ya magendo. Akizungumza katika ziara ya naibu waziri wa fedha na uchimi Pereira Ame Silima alielitembelea tawi hilo, Mwimo ameishauri serikali kutekeleza nia yake ya kuruhusu wafanyabiashara kununua zao hilo. Hata hivyo amesema shirika la biashara la Zanzibar ZSTC linalonunua zao hilo, libaki kama mwangalizi mkuu na sio mnunuzi. Aidha Mwimo amesema ukuwaji mdogo wa sekta ya kilimo umeleta athari ya upatikanaji wa chakula na kuongezeka mfumko wa bei wa bidhaa.

Hivyo ameishauri serikali kuimarisha sekta ya kilimo kwa kukiwekea miundombinu ya umwagiliaji maji na kuwapatia wakulima mbegu na pembejeo. Naibu waziri Silima amewataka watendaji wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuwa wafanisi katika ukusanyaji wa mapato na kubuni vyanzo vingine vya kulingizia fedha taifa. Akizungumza na watendaji wa TRA huko msikiti Mabuluu amesema ukusanyaji wa mapato ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi. Katika ziara hiyo naibu waziri huyo alitembelea tawi la benki kuu Zanzibar, Idara ya Forodha na mamlaka ya mapato Tanzania TRA.

WALIOVUNJIWA MTOPEPO 1996 WATISHIA KUISHTAKI SMZ

Wananchi waliovunjiwa nyumba zao katika maeneo ya Mtoni Kidatu wametishia kuishtaki serikali ya Mapinduzi Zanzibar endapo hawatalipwa fidia baada ya kubainika nyumba zao zilivunjwa kimakosa.

Mwenyekiti wa kamati ya waathirika hao Ali Shamte Nahodha amesema tokea nyumba zao walipovunjiwa mwaka 1996 hadi sasa hajalipwa fidia licha ya kuahidiwa na serikali kulipwa.

Amesema kamati hiyo ilimuandikia barua katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi, na kutakiwa wasubiri katika kipindi kifupi, lakini hadi sasa bado hawajalipwa.

Mwenyekiti huyo amesema kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 wamekuwa wakifuatilia malipo yao, huku wengine wakiwa wameshafariki dunia na waliobaki wanaendelea kuhangaika kutokana na kukosa makazi.

Kwa mujibu wa Nahodha ripoti iliyotolewa na tume iliyokuwa ikishughulikia muafaka mwaka 1998 ilitaka wathirika hao walipwe fidia ya thamani ya nyumba zao kufuatia kufanywa tathmini.

Jumla ya nyumba mia saba na 72 zilivunjwa katika eneo la Kidatu Mtoni tokea mwaka 1996 wakati wa utawala wa Dr. Salim Amour Juma kwa madai sehemu hiyo  haikuruhusiwa kujengwa nyumba za kuishi watu