Mtabiri wa Afrika Mashariki Sheikh Yahya Hussein

Mnajimu na Mtabiri maarufu Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein amefariki dunia asubuhi hii jijini Dar es Salaam. Akizungumza na mwandishi wetu mtoto wa marehemu Hassan Yahya Husein  amesema ”babayake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu.” ”Aliamka asubuhi ya leo akiwa buheri wa afya, akaanza kazi yake ya kuwaona wenye matatizo wanaokuja kwake. ” Kama kwenye saa 3.00 asubuhi hivi, akaanza kujisikia vibaya, akapewa glasi ya juisi lakini hali haikutulia”. ”Tukaamua kumkimbiza katika hospitali moja maeneo ya Morocco na alipofikishwa hapo madaktari wakasema tayari ameshafariki dunia”.

Advertisements