Uingereza imeahidi kuimarisha ushirikiano wa  biashara na Zanzibar kwa manufaa ya pande mbili hizo.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika Henry Bellingham ameyasema hayo Ikulu mjini Zanzibar alipokuwa akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,

Amesema kuwepo serikali ya Umoja wa Kitaifa imesaidia kuleta amani na utulivu jambo ambalo limewafanya wawekezaji na wafanyabiasahara wavutika kuweka vitega uchumi vyao Zanzibar.

Waziri huyo amesema Utalii na Biashara ni miongoni mwa mambo yatakayoekezwa na waekezaji wa Uingereza na kuahidi kuwahamasisha waekezaji na wafanyabiashara wa nchi hiyo waje kuekeza Zanzibar.

Nae Dk. Shein alimueleza waziri huyo Zanzibar imejiandaa kuwakaribisha wawekezaji na imeweka mazingira mazuri.

Aidha, Dk. Shein aliahidi kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Zanzibar na Uinmgereza ili kuleta maendeleo kwa nchi zote mbili.

Advertisements