MAKAMU wea kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim seif Sharrif Hamad amesema Serikali inalenga kuzichukulia hatua za kisheria mara moja, taasisi zote zinazoshughulikia usafirishaji wa Mahujaji, zitakazobainika kwenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.
Maalim Seif ametoa indhari hiyo jana wakati alipozindua Taasisi ya kusafirisha mahujaji ya ‘Ahlu Sunna Waljamaa Hajj & Trust” katika ukumbi wa Jaffery Complex, jijini Dar es Salaam katika hafla iliombatana Kongamano la waislamu kuhusu Hijja.
Amesema kuna taarifa za kuthibitisha kuwa baadhi ay taasisi za kusafirisha mahujaji nchini, zimekuwa zikiwatendea vitendo visivyokubalika watu wanaojiandikisha kwa safari za Hijja, kwa kuwatelekeza katika viwanja vya ndege na nyingine kuwanyima hata chakula kinyume na ahadi zao.
Alisema inasikitisha kuona waumini wa kiislamu wakitafuta fedha kwa juhudi kubwa ili kukamilisha nguzo hiyo muhimu ya uislamu, lakini hatimae hukumbana na masahibu kadhaa kutoka taasisi hizo, na kuifanya ibada yao kuingia dosari.
Alisema Serikali haitasita kuingilia kati mara moja pale itakapobaini kuwepo kwa taasisi inayokwenda kinyume na ahadi ilizotoa wakati wa kusaka mahujaji.
Maalim Seif alitumia Kongamano hilo kuziomba tasasisi za fedha kuanzisha Akaunti maalum zilizo katika mfumo wa Benki za kiislamu ili kuwawezesha waumini wa dini ya kiislamu kudunduliza fedha na hatimae kwenda Makka kuhiji.
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka Masheikh nchini kote, kupitia mihadhara wanayoiendesha, kuwashajiisha waislamu, kufanya utafiti na kuwa na mikakati ya kulipatia ufumbuzi tatizo la Tanzania kuwa na mahujaji wachache, ikilinganishwa na idadi kubwa ya taasisi za kusafirisha mahujaji.
Alisema kumekuwepo na dhana potofu miongoni mwa vijana kuchelewesha kwenda Hijja hadi malengo yao ya kidunia yakamilike na kupelekea kuwapa usumbufu mkubwa watu wanaowahudumia wakati wanapozeeka.
Vile vile alisema kuna baadhi ay wazee hukusanya mali nyingi kwa ajili ya watoto wao lakini pale wanapofariki, watoto hao hawakumbuki haki za Mwenye Mungu juu ya mali walioirithi, wakijua kuwa wazazi hao hawakukamilisha ibada ya Hijja kama walivyoamrishwa.
Katika hatua nyingine Maalim Seif, alilaani vikali tabia ya ugonvi katika misikiti, inayotokea kati ya wazee na vijana wenye itikadi tofauti, miongoni mwao wakiwemo wazee waliokwisha kuhiji, hali inayothibitisha kutokufahamuj falsafa ya kwenda Hijja.
Alifafanua kuwa misikiti ni mahala pa kusimamisha uislamu pamoja na kuwaunganisha waislamu na sio mahala pa ugomvi.
Mapema Katibu Mtendaji katika Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana, Sheikh Abdalla Twalib, alisema Tanzania ina idadi kubwa ya waislamu wenye uwezo wa kwenda kuhiji pamoja na kuendeleza dini, lakini
hawajashajiishwa ipasavyo kutumia rasilimali zao katika kukuza dini.
Aliasema ili kufikia lengo la kupeleka Mahujaji 30,000 kama fursa inavyotoka, kuna haja ya kumuelekea Mwenyezi Mungu, kuwa wawazi pamoja na kutekeleza ahadi kwa mahujaji.
Mapema Masheikh mbali mbali kutoak mikoa ya Tanzania Bara walitoa mawaidha pamoja na mada katika hadhara hiyo, ikiwemo Risala ya utukufu wa hijja katika uislamu na Falsafa ya Hijja na Umoja wa Kiislamu.
Walisema robo tatu ya Watanzania wanaokwenda Hijja kila mwaka huwa ni wazee kutokana an tabia iliojengeka miongoni mwa waislamu ya kusubiri hadi wakamilishe mambo yao ya kidunia.
Walisema changamoto kubwa inayoikabili jamii ya kiislamu wakati huu pale mtu anapozikwa, ni kuwa ndugu wa marehemu hutangaza madeni ya Marehemu na kusahau deni la Mwenyezi Mungu, kwa mja wake.
Walianisha kuwa ni jambo baya kwa wafiwa kukimbilia kugawana mali za Marehemu na kusahau deni alilonalo kwa Mola wake.
L

Advertisements