Benera ya Zanzibar (Zanzibar Flage)

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 613 katika mwaka wa fedha 2011/2012 ambazo ni ongezeko la shilingi bilioni 169 katika bajet ya mwaka unaomalizika 2010/2011. Akitoa muhutasari wa bajeti mpya kwa wandishi wa habari waziri anaeshughulikia masuala ya fedha na uchumi Omar Yussuf Mzee amesema kati ya fedha hizo shingili bilioni 340 ni ruzuku na mikopo kutoka kwa wahisani na zilizosalia zitakusanywa kupitia vyanzo vya mapato vya ndani. Mzee amesema bajeti ya mwaka huu imetenga fedha nyingi kwa ajili ya matumizi ya mipango ya maendeleo na zilizosalia zitapelekwa katika utekelezaji wa shughuli za serikali. Amesema kutengwa kwa fedha nyingi katika mipango ya maendeleo ni kutaka kuwavutia vijana kujingiza katika sekta ya kilimo kwa vile wengi wao wameachana nacho kutokana kukosa tija. Waziri Mzee pia amesema bajeti mpya itawangalia watalamu wazalendo kwa kuwandalia mazingira ambayo kila mmoja ataweza kufanya kazi Zanzibar. Bajet hiyo itasomwa kwa ukamilifu katika kikao cha baraza la wawakilishi kitakachoanza Juni 15 mwaka huu huko katika ukumbi wa baraza hilo Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Advertisements