MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR MHE, BALOZI SEIF ALI IDDI AKIWA NA MSHANGAO MKUBWA KUFUATIA KUTOKUWEPO MUASHAJI WA ZAMU WA JENERETA LINALO HUDUMIA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA, BALOZI SEIF ALIFANYA ZIARA YA HAFLA USIKU HOSPILINI HAPO NA KUBAINI BAADHI YA KASORO ZA KITENDAJI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi amekemea vikali tabia isiyoridhisha ya baadhi ya wahudumu wa afya katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja ya kuhatarisha maisha ya wananchi wenzao kwa kutowajibika ipasavyo. Mheshimiwa Balozi Seif Iddi alitoa kauli hiyo alipofanya ziara ya ghafla usiku hospitalini hapo, kufuatia shutuma na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo visivyoridhisha hospitalini hapo na utoaji mbaya wa huduma uanofanywa na baadhi ya watendaji. Alisikitishwa, kushangazwa na kukasirishwa na kitendo cha Fundi wa jenereta kutowepo kazini wakati umeme ulipokatika na kusitisha huduma zote za hospitali hadi alipofuatwa nyumbani kwa gari la kuchukulia wagonjwa baada ya muda wa zaidi ya nusu saa. Mheshimiwa Makamu huyo wa Pili wa Rais alisema kitendo hicho kimeonesha dharau kazini na kingeweza kusababish vifo kwa waliokuwa wakihudumiwa kwa wakati huo. Hata hivyo alieleza kuridhishwa kwake na baadhi ya Madaktari na wahudumu wengine kwa namna wanavyochapa kazi sambamba na jitihada za Serikali za kudumisha huduma hiyo na kuwataka waongeze bidii wakati Serikali inajitahidi kuimaisha mazingira yao. Alisisitiza haja ya uvaaji wa uniform kazini ili waonekane nadhifu na kuwatafautisha na watu wa kawaida wanaoingia bila ya mpango na kusababisha vurugu kwa wagonjwa Mawodini. Kuhusu uimarishaji wa huduma hizo Daktari wa zamu katika wodi mbili za Surgical Dr Abdulrahman Yussuf aliyekuja kwa mazoezi ya vitendo kutoka Bara alisema ametiwa moyo na jitihada za SMZ za kuimarisha huduma pamoja na za kwao na kusema yuko tayari kufanyakazi Zanzibar baada ya kuhitimu Chuo

Advertisements