Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepandisha kima cha chini
cha mishara kwa asilimia 25.

Waziri wa nchi ofisi ya rais, utumishi wa umma na
utawala bora Haji Kheri amesema wafanyakazi wa ngazi nyengine mishahara yao itaongezwa kuzingatia elimu na muda wa utumishi kazini

Akiwasilisha hutuba ya bajeti ya wizara hiyo katika kiako cha baraza la wawakilishi amesema upandishaji huo wa mishahara umezingatia pia nyongeza walizozikosa wafanyakazi tokea mwaka 2007.

Hata hivyo waziri Kheir amesema kwa kuzingatia ufinyu wa bajeti utekelezaji wa mabadiliko hayo ya mishahara mipya bila ya malimbikizo utafanywa kuanzia mwezi Octoba mwaka huu.

Amefahamisha kuwa mabadiliko hayo ya mishahara yanakwenda sambamba na utekelezaji wa ahadi za rais Dk Ali Mohd Shein aliyoitoa ya kuinua maisha ya wafanyakazi katika kampeni yake ya uchaguzi mkuu Octoba mwaka jana.

Waziri Kheri, amewasihi   wfanyakazi   kujenga ari  ya kuongeza  juhudi  na maarifa   katika kutoa huduma  bora   katika mchakati  wa kuimarisha uchumi na maendeleo  ya Taifa.

Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeomba kuidhinishiwa shiling billion nne, mulioni 855 laki mbili na elfu 46 kwa mwaka wa fedha 2011/2012 kwa ajili ya matumizi ya ofisi hiyo

Advertisements