Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepandisha bei ya kununulia karafuu kavu kutoka kwa mkulima kwa zaidi ya asilimia 100 kutoka bei ya msimu uliopita ya shilingi elfu tano kwa kilo moja. Akitangaza bei hiyo kwa wandishi wa habari mjini hapa waziri wa biashara, viwanda na masoko Nassor Ahmed Mazuri amesema serikali imeamuwa kulipa wakulima asilimia 80 ya bei ya kuzia karafuu katika masoko ya kimataifa. Akitangaza bei hizo ya kufungulia ununuaji wa karafuu kwa msimu huu utakaozinduliwa baadae mwezi huu waziri Mazurui amesema…Gred 1 ni shilingi 10,000/-, grade2 ni shilingi 9500/- na gradi 3 ni shilingi 9000 kwa kilo moa.

Waziri Mazuri amesema bei hiyo imekuja baada ya serikali kufanya utafiti wa mwenendo wa bei ya karafuu katika masoko ya dunia kwa lengo la kuandaa bei muafaka itakayoleta tija kwa wakulima. Amesema pamoja na serikali kutangaza bei hiyo pia imeandaa mkakati wa kulinda bei hiyo iwapo yatatokea mabadiliko katika soko la dunia yatakayosababisha kushuka kwa bei hiyo. .Amefahamisha iwapo karafuu itashuka katika soko la dunia hakutakuwa na karafuu itakayonunuliwa chini ya bei iliyotangazwa kutoka kwa mkulima na ikiwa bei itapanda katika soko hilo bei kwa mkulima itapanda kwa asilimia 80. Waziri Mazuri amesema kutokana na bei hiyo mpya, serikali haitarajii kuona baadhi ya wakulima wakiuza karafuu zao kwa njia ya magendo. Amesema tangazo hilo la serikali la kuongeza bei ya kununulia karafuu kwa zaidi ya asimia 100 ina lengo la kuendeleza zao hilo na kuimarisha uchumi wa wakulima na serikali kwa ujumla. Kuhusu kubinafsishwa kwa zao hilo waziri Mazuri amesema kwa hivi sasa serikali haina mpango huo kwa vile imedhamiria kufufua zao hilo badala ya kubinafsisha… Msimu uliopita serikali ilununua karafuu kavu kutoka kwa wakulima kwa shilingi elfu tano hadi 7,500 kwa kilo ambazo zaidi ya tani 2,000 zilinuliwa na shirika la biashara la serikali ZSTC. Kwa mujibu wa waziri Mazuri msimuu huu utakaoanza katikati ya mwezi ujao serikali inatarajia kununua zaidi ya tani elfu tatu kutoka kwa wakulima ambapo miaka ya 80 Zanzibar ilikuwa ikisafirisha karafuu nje ya nchi kwa zaidi ya tani elfu 12 kwa mwaka

Advertisements