Wizara ya afya Zanzibar imesema inakabiliwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaotaka kusafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa wizraa hiyo Juma Duni Haji amesema licha ya kuimarika huduma za afya katika hospitali nchini, lakini bado wagonjwa wengi wanashindwa kupatiwa matibu.

Amesema kutokana na hali hiyo wizara hulazimika kuwaombea misaada ya kifedha wagonjwa hao ili kuwapaleka nje ya nchi hasa wale wanaougua maradhi ya moyo, figo na saratani.

Duni amesema katika kipindi cha mwaka 2010/2011 wagonjwa 60 walipelekwa nje ya nchi na kuwafanya wagonjwa wengi kukwama na wengine kupoteza maisha kutokana hali mbaya ya fedha.

Amesema hivi sasa wakati anasoma hutuba hiyo mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi kuna zaidi ya wagonjwa 190 wanaosubiri fedha kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo Zanzibar hayapo.

Waziri Duni amesema ili kupunguza idiadi hiyo ya wagonjwa kusafirishwa nje ya nchi wizara inaendelea kuimarisha hospitali ya kuu ya Mnazi mmoja ili kuwa hospitali ya Rufaa.

Amesema katika mpango huo utahusisha upatikanaji wa madaktari bingwa na vifaa vinavyohitajika ili kutoa huduma hizo ambazo awali zilikosena.

Katiba hutoba hiyo ya bajeti wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa zaidi ya shilingi bilioni 13 kwa mwaka wa fedha 2011/2012, huku ikipangiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 537.

Advertisements