Kiasi ya watoto elfu moja imebainika wanabakwa kila mwaka hapa Zanzibar na chini ya watoto 50 hufanyiwa vitendo hivyo kila mwezi.

Akizungumza na Zenji fm radio Daktari wa kituo cha Mkono kwa Mkono kiliopo katika hospitali ya Mnazi mmoja Dr. Marijani Msafiri amesema wengi ya watoto wanaofanyiwa udhalilishaji huo ni watoto wenye umri chini ya miaka 16.

Dr. Marijan amesema vitendo hivyo vinawasababishia watoto hao kushindwa kuendelea na masomo yao kutokana na kuathirika kiakili na kisaikolojia kutokana kufikiria mara kwa mara vitendo hivyo waliofanyiwa.

Aidha Dr. Marijan amesema lengo la kuanzishwa kituo cha mkono kwa mkono katika hospitali ya Mnazi mmoja ni kutoa huduma kwa ajili ya kupata ushihidi utakaowatia hatiani watu wanashukiwa kufanya vitendo vya ubakaji dhidi ya watoto.

Wakati huo huo mtandao wa wanahabari Tanzania unaojumuisha watoto kutoka Unguja na Pemba umelaani matukio ya ubakaji dhidi ya watoto ambayo yamekithiri hapa Zanzibar.

Mtandao huo unaojumuisha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na virusi vya ukimwi wametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea kituo cha mkono kwa mkono.

Advertisements