Mizengo Peter Pinda

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda amesema mfumo wa sasa wa muungano ni mzuri na kusema hatua yoyote itakayobadili mfumo huo ni utahatarisha uimara wa muungano wenyewe.

Akijibu maswali ya papo kwa pao bungeni mjini Dodoma amesema kwa vile marekebisho ya katiba yatafanyika wananchi watakuwa na fursa ya kuchagua mfumo unaofaa ambao utakuwa na maslahi kwa pande mbili.

Hata hivyo amesema mfumo wowote wa muungano utakaoziweka Tanzania bara na Zanzibar katika hali ya kufanana mfumo huo utakuwa mgumu kuutekeleza kutokana na idadi ya watu ya kila upande.

Hivyo waziri mkuu Pinda amewataka watanzania kuendelea kudumisha muungano kwa kuangalia matatizo yanayoukabili kwa umakini badala ya kutumia jazba

Kipindi hicho cha maswali na majibu ya papo kwa papo kimechukua muda mkubwa wa hoja za masuala ya muungano, umeme na mafuta.

Advertisements