Wizara ya miundo mbinu na mawasiliano inaendelea na mazungumzo na kampuni nne za kigeni zinazotaka kuwekeza katika usafiri wa ndani wa baharini  ili kupunguza tatizo la usafiri kati ya Pemba na Unguja.

Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri wa wizara hiyo Ussi Haji Gavu amesema moja ya kampuni hizo kutoka Italia ujumbe wake ulitarajiwa kuwasili Zanzibar leo kwa ajili ya mazungumzo.

Amesema kampuni nyingine  ya Uturuki, Sazana na kampuni kampuni ya Dubai zimeonesha nia ya kushirikiana na serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kutatua tatizo la usafiri kati ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha Gavu amesema kwa sasa wizara ya miundo mbinu na mawasiliano inafanya mazungumzo na wamiliki wa vyombo vya ndani kuongeza usafari kati ya Unguja na Pemba ili kupunguza tatizo hilo

Kauli hiyo ya wizara ya miundo mbinu kukaribisha wawekezaji wa kigeni wa shughuli za usafiri wa baharini kati ya Unguja na Pemba imekuja huku kukiwa na malalamiko ya baadhi ya vyombo vinavyotoa huduma hiyo vimechakaa na kutishia usalama wa abiria.

Advertisements