Ali Juma Shamhuna

Waziri wa ardhi, makaazi, maji na nishati Ali Juma Shamhuna amesema uhaba wa umeme ulioko Tanzania bara hauwezi kuathiri uletaji wa nishati hiyo kwa kisiwa cha Unguja kutokana na mikataba iliyosainiwa. Akijibu suala la nyongeza katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema ni kweli Tanzania bara inakabiliwa na umeme mdogo kuliko matumizi ya wananchi, lakini mgao uliopo hauhisiani na Zanzibar. Shamhuna amesema shirika la umeme Tanzania liko tayari kuongeza kiwango cha umeme unaohitajika kwa sasa cha Megawati 45, lakini kuna hofu ya kuunguza waya unaopita chini ya bahari kutokana na kuchakaa

Kuhusu ununuzi wa majenerata uliofanywa na serikali huku ikijua uwezo wa kueyaendesha ni mdogo, Shamhuna amesema majenerata hayo yalinunuliwa katika kipindi cha shida, hivyo haikufikiriwa gharama za uzalishaji.

Amesema majanareta hayo yanatumia mafuta ya disel yasiokuwa na sulpha ambayo ni ghali na uzalishaji wa uniti moja ya umeme unagharimu shlingi 250 wakati umeme wa kawaida bei ni shilingi 130.

Hata hivyo waziri Shamhuna amesema shirika la umeme Zanzibar limeomba kuongeza bei ya Unit au kupewa ruzuku serikalini la si hivyo shirika hilo litashindwa kuendesha majenerata hayo kwa hasara. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilinunua majenerata 20 yenye uwezo wa kuzalisha Megawati 20 za umeme wakati ihuduma ya umeme ilipokatika kwa kipindi cha miezi mitatu, lakini majenerata hayo yameonekana ni mzigo kutokana na kuendeshwa kwa hasara.

Advertisements