Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeongeza bei ya karafuu kwa wakulima.

Bei mpya sasa kwa karafuu daraja la kwanza kwa kilo itakuwa shilingi 15,000/- ni sawa shilingi 22,000/- kwa Pishi

Shirika la Biashara la Taifa(ZSTC) litanunua karafuu daraja la pili kilo moja kwa shilingi 14,000 ni sawa na Shilingi  21,000/ kwa Pishi  na Karafuu daraja la tatu itanunuliwa kwa kilo moja shilingi 14,000/- ni sawa na shilingi 21,000/- kwa Pishi.

Wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa Serikali na kuuza Karafuu zao ZSTC kwa ajili ya kupiga vita magendo na kuinua uchumi wan chi.

Meneja Mkuu wa ZSTC,Suleiman Jongo amesema kutangazwa kwa bei mpya na Shirika lake ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein katika mazungumzo aliyofanya na wakulima wa karafuu Kisiwani Pemba.

Serikali imeongeza bei ya ununuzi wa karafuu baada ya mwenendo wa bei ya karafuu katika soko la dunia kubadilika na itakuwa ikifanya hivyo kadri ya mwenendo wa bei katika soko la dunia itakavyokuwa.

Aidha, ZSTC inasisitiza kuwa bei ya makonyo ni shilingi 1500/- kwa kilo na bei ya mchumaji isipunguwe shilingi 2,000/- kwa Pishi.

Advertisements