Muimbaji mkongwe wa muziki wa taarab  nchini Abdullah Issa  ametangaza rasmi kujitoa katika fani hiyo baada ya kuimba kwa muda wa miaka 45 na kupiga marufuku kutumika kwa nyimbo alizoziimba .

Akizungumza na Zenji fm radio  mkongwe huyo amesema mbali na kutangaza kuachana na fani hiyo ya muziki wa taarabu pia amesitisha kutumika kwa njimbo zake zote katika vyombo vya habari na matumizi ya nyumbani pamoja na  katika kumbi mbalimbali za starehe.

Hivyo ameeleza kuwa endapo mtu ama taasisi yeyote itaamua kutumia nyimbo zake hizo hatua kali za sheria atachukua juu yake  kutokana na sasa kuamua sauti yake hiyo kwa mambo ya kheri

Advertisements