Wizara ya kilimo na mali asili Zanzibar imepiga marufuku ingizaji wa bidhaa ya ndizi, miche ya migomba, majani na vigogo vya mgomba  kutoka tanzania bara kutokana na kuibuka maradhi ya kunyauka migomba.

Mkuu wa kitengo cha uhifadhi na utibabu wa mazao kutoka wizara hiyo Zainab Saliim Abdallah amesema maradhi hayo yanasababishwa na baktiria yameingia Tanzania bara tokea mwaka 2007.

Hata hivyo amesema maradhi hayo hayana athari kwa mlaji, na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutoa taarifa kwa watu watakaokiuka marufuku hiyo.

Zainab amesema kitengo hicho kimekamata ndizi zilizobainika kuwa na maradhi hayo kutoka bara na mipango yakuziangamiza inaandaliwa.

Advertisements