Archive for September, 2011

TANI 789 ZA KARAFUU ZENYE THAMANI YA ZAIDI BILIONI 11 ZANUNULIWA PEMBA

Jumla ya tani 789 za karafuu zimenunuliwa hadi kufikia jana zenye thamani ya Shs billion 11 million 631 laki nane sabiini na saba elfu mia mbili na hamsini.

 

Ununuzi huo ni kuanzia kipindi cha Mwezi wa Julai hadi hapo jana ambapo karafuu zote hizo zimeuzwa katika Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC) katika vituo mbali mbali kisiwani Pemba.

 

Akitoa taarifa leo mbele ya Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Fedha Biashara na Kilimo Zanzibar huko katika ofisi ya ZSTC Wete Pemba Afisa Mdhamini wa Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Hemed Suleiman Abdallah, amesema kuwa ununuzi huo umetokana na mashirikiano yaliyopo kati ya wakulima na ZSTC.

 

Akielezea mchanganuo wa ununuzi wa karafuu hizo amesema kuwa kwa Mkoa wa Kusini Pemba Wilaya ya Mkoani imenunua Tani 402 sawa na shs Bilion 5.9, Wilaya ya Chake Chake Tani 184 sawa na shs Bilion 2 na Milion 72.

 

Kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Wilaya ya Wete imenunua Tani 155 sawa na Bilion 2 na Milion 31 na Wilaya ya Micheweni Tani 45 sawa na Milion 68 Sitini na tisa elfu, elfu mbili mia tisa na sabiini na tano.

 

Amesema kuwa wananchi wa Pemba wametambua athari ya magendo ya Karafuu hivyo wamehamasika kuuza karafuu zao katika vituo vya ununuzi vya ZSTC kwa kutambua umuhimu wa kupeleka zao hilo huko kwa faida ya maendeleo ya Zanzibar.

 

Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi ya Fedha, Biashara na Kilimo, Salmin Awadh Salmin amelipongeza Shirika la ZSTC kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kufanikisha ununuzi wa tani hizo tokea kuanza msimu wa ununuzi wa karafuu mwezi Julai mwaka huu.

 

Amesema kuwa ZSTC imepiga hatua kubwa kwa kusimamia upatikanaji wa Tani hizo kwani imeonesha tofauti kubwa ya ununuzi wa karafuu hizo ikilinganishwa na msimu uliopita.

 

Salmin Awadh Salmin amewataka ZSTC kuwahamasisha wananchi kupanda Mikarafuu mipya na kuzidisha kutoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha karafuu zao wanazozipeleka ZSTC zipo katika hali nzuri ili waweze kupata daraja la kwanza kwa faida zaidi.

 

Wajumbe hao walitembelea ofisi kuu ya ZSTC iliyopo Wete, Banda la Karafuu la Wete vituo vya ununuzi wa karafuu vya Mzambarauni na kituo cha ununuzi cha Wete kisiwani Pemba.

 

Advertisements

TUME YA KUCHUNGUZA AJALI YA MELI YA SPICE ISLENDER YATANGAZWA

Serekali yaMapinduzi ya Zanzibar imetangaza kamati ambayo atafanya uchunguzi wa ajali ya meli ya MV spice islanders  iliyotokea ikiwa safarini kueleka Pemba na kusababsha vifo vya watu 203.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  na katibu wa Baraza la Mapinduzi na katibu mkuu kiongozi, dkt. Abdulhamid Yahya Mzee inaeleza kwamba  kwa kutmia uwezo alipewa chini ya sheria ya Tume  za Uchungzi  sura ya 33  ya sheria ya Zanzibar ,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Braza la Mapinduzi dkt,Ali  Mohd Shein  ameunda tume hiyo.

 

Tume hiyo ambayo ina wajumbe kumi iatongozwa chini ya mwenyekiti Jaji  Abdulhakim Ameir Issa ambaye ni mwanasheria mzoefu na kwa sasa ni jaji wa Mahkama kuu ya Zanzibar .

 

Wengine ni Jenerali S,S  Omar ambaye yeye ni mkuu wa jeshi la wanamaji katika jeshi la wananchi  wa Tanzania (JWTZ),COMDR. Hasan Mussa  Mzee  ni mkuu wa kikosi cha wanamaji wa KMKM na Kepten Abdulla Yusuf Jumbe  ni nahodha  mzoefu  meli kitifa na kimataifa  ambapo pia aliwahi kuwa nahodha wa mv Mapinduzi iliyokuwa inamiloikiwa na Serekali ya Zanzibar.

 

Vile vile kamati hiyo imemuhusisha  Cpten  Abdaulla Juma Abdulla mwanamaji mstaafu  sasni naibu katibu Mkuu  Ofisi ya rais  idara maalum za SMZ ,Salum Taufik Ali  ni mwanasheria mzoefu pia anauzoefu wa sheria za bahari kwa sasa ni mwanasheria wa Zantel.

 

 

Kapten Hatibu Katandula  ni mkufunzi mkuu wa  katka chuo cha baharia  ch Dar Salam na  Bi Mkakili  Fauster Ngowi ni wakili katika  Ofisi  ya Mwanasheria  Tanzania  ,mwanajeshi mstaafu Ali Omari Chengo na alikuwa mjumbe wa Baraza la waakilishi  na Naibu Waziri  wa NM awasiliano  katika Serekali ya Mapinduzu siku zilizo pita.

 

Na wa mwisho ni katibu wa tume hiyo  Shaabani Ramadhani  Abdulla ni mtaalamu wa  wa sheria z bahari ,na hivi sasa ni mwanasheria katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Znazibar (DPP).

 

Tume hiyo imeindwa ilikujuwa ukweli  kuhusu kutambuwa  chanzo cha  ajali ya meli  hiyo ya iliyosababisha maafa makubwa na simanzi kubwa katika visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

 

 

 

HAKUNA WA KULAUMIWA AJALI YA MV SPICE ISLANDER-DR. SHEIN

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Moh’d Shein, amesema huu sio wakati wa kulaumiana na kushtumiana kutokana na Msiba mkubwa uliolipata Taifa kwa kupoteza mamia ya Wananchi kwa kuzama Meli ya Mv, Spice Islandar.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa mkoa wa Kusini Pemba amewataka wananchi kuwa na subira na mshikamano juu ya tukio hilo huku serikali ikiendelea na juhudi za uokozi na uchunguzi wa ajali hiyo.

Dr. Shein amesema msiba huo utabaki historia kutokea katika Visiwa vya Zanzibar tangu kuanza kwa Safari za Meli katika Karne zilizopita.

Amesema msiba huo sio wa Wazanzibar peke bali ni wa Taifa zima la Tanzania kwa vile kila mmoja umemgusa kwa namna moja ama nyengine.

Dk. Shein aliwataka Wananchi wa Zanzibar, kuzidi kushirikiana na kusaidiana na kuonesha utulivu kama waliouonesha katika kipindi cha kutokea ajali ya meli ya Mv Spice Islander.

kwa Mtihani huo kwani yote yaliotokea ni muandiko wa Mwenyeezi Mungu Pekee.

 

Alifahamisha kuwa Serikali zote mbili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano kwa pamoja zilishirikiana na Wananchi mbali mbali ilikuona wanakabiliana na Janga hilo kwa Uokozi wa Watu na kuwazika wale wote walifariki Dunia kila mmoja na Kaburi lake,

 

“ Tulizika maiti zote huko Kama Unguja , kwa vile hatukuwa na namna nyengine kwani Maiti wa maji ya bahari haekeki na Uwezo wa Chumba cha kuhifadhia Maiti katika Hospitali ya Mnazi Mmoja hakina Uwezo mkubwa kwa wakati mmoja na wale maiti walikuwa wengi.” Alieleza Dk, Shein.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk, Ali Moh’d Shein, alieleza kuwa Serikali imejifunza mengi kutokana na Msiba  huo , na itajitahidi kuona suala kama hilo halitokei tena .

 

Aliwahakikishia Wananchi kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, imeazimia kuunda Tume maalumu ilikuchunguza Chanzo cha ajali hiyo , na kuchukuwa ripoti ya uchunguzi huo na hatimae kuchukuwa hatua bila ya upendeleo wala kumuonea mtu.

 

“ Tume tutakayoiunda tutaitangaza haraka sana katika saa zijazo na itafanya kazi bila woga na bila ya kumuonea mtu yoyote” alisema Dk Shein.

 

Aliendelea kusema kuwa kwa kusaidiana na Wahisani na Wafanyabiashara mbali mbali , Serikali imejiandaa kukabiliana na hali kama hiyo kwa kuwataka Wafanya biashara kuekeza katika usafiri wa Baharini kwa kutafuta Meli kubwa itakayo ondowa shida ya usafiri kati ya Pemba na Unguja.

 

“ Pale Serikali itakapo kuwa na uwezo itafanya juhudi ya kumiliki Meli yake wenyewe , hapo siku za nyuma srikali ilikuwa ikimiliki meli mbili mbili, kubwa na ndogo…..ilikuwa na usafiri wa uhakika kwa Wananchi wa Unguja na Pemba”alisema Dk. Shein.

 

Alieleza kuwa pamoja na Serikali kufanya wajibu wake mbali mbali , lakini haija sita kufanya hivyo na inaungana na Wananchi wa Pemba , kwa mtihani huo na amewataka kuwa na subra kwani liliandikwa na Allha halina budi kufanyika .

 

Hivyo  aliwashukuru Watendaji wakuu wa Serikali na Taasisi mbali mbali kwa ujumla kwa kazi kubwa waliochukuwa za kukabiliana na Janga hilo kubwa na nchi ikiwa iko katika hali ya Utulivu.

 

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa srikali imejifunza mambo mengi katika tukio hilo na kueleza lengo lake hivi sasa la kujipanga vizuri huku kukiwa na mashirikiano mazuri pamoja na ahadi mbali mbali za kuunga mkono juu ya jambo hilo kutoka kwa washirika wa maendeleo katika kuweka mikakati zaidi.

 

Nao wananchi na viongozi hao walisifu juhudi za serikali chini ya uongozi wa Dk Shein katika kukabiliana na tukio hilo.

 

Aidha, walieleza kuwa wanaungana na Rais kueleza kuwa huo ni msiba kutoka kwa Allah na kueleza kuwa kama Qur-an na hadithi za Mtume zinavyosisitiza subira basin a wao wamo katika kutekeleza amri hiyo ya Mola wao na Mtume wao Muhammad S.A.W.

 

Kwa mujibu wa uongozi wa Wilaya ya Mkoani ulieleza kuwa watu waliofariki ni 31 na 4 waliokolewa na kwa Wilaya ya Mkoani ni 146 walifariki ambapo kwa Shehia ya ziwani peke yake waliofariki ni 56

MAITI TANO ZA AJALI YA MELI ZANZIBAR ZAOKOTWA MOMBASA

Maiti nyengine tano za ajali ya meli ya Spice Islanders wamepatikana eneo la Shimoni Mombasa na kulazimka kuzikwa kwenye eneo hilo kutokana na hali zao.

Kwa mujibu wa taarifa wa balozi mdogo wa Tanzania nchini Kenya Yahya Haji Jecha amesema kuanzia jana maiti zimeanza kupatikana eneo la shimoni Mombasa.

Amesema kati ya maiti hizo nne ni za wanaume na moja ni ya mwanamke ambapo maiti hizo zimedaiwa kuwa zimeharika sana ambazo zisingeweza kusafirishwa

Katika hatua nyingine

Kazi za ukozi za kuipata miili mingine kutoka kwenye meli ya Spice Islander iliyozama mwishoni mwa wiki huko Nungwi imesitishwa kwa muda kutoka na hali mbaya ya hewa.

Taarifa kutoka Nungwi zinasema wapiga mbizi wa ndani na wale kutoka Afrika ya kusini wamesitisha kwa muda shguhuli za ukozi kutokana na bahari kuchafuka.

Wakati huo huo usafiri wa baharini kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam umetatizika kutokana na vyombo vya usafiri kuwa kidogo baada ya kutokea ajali ya meli ya Spice Islander.

Hata hivyo nauli za vyombo hivyo zimeripotiwa kupanda

BAADHI YA MAITI ZA AJALI YA SPICE ZAONEKANA KENYA

Baadhi maiti za watu zinazosodikiwa kutoka kwenye meli ya Spice Islander iliyozama mwishoni mwa wiki iliyopita zimeanza kuonekana katika mwambao wa pwani ya Kenya.

Akizungumza na Zenji Fm radio mkaazi wa kijiji cha Moa, Tanga Bakar Bunda amesema zaidi ya maiti sita zimeonekana zikielekea katika pwani ya kijiji hicho kilichokuwa karibu na Kenya.

Amesema kitambulisho chenye jina la Masoud Shaaban Hamad mkaazi wa Mtambwe kimeokotwa kikiwa ndani ya begi dogo na wavuvi wa kijiji hicho

Aidha Bunda amesema wamepata habari kutoka nchini Kenya kuna maiti nyingine zinazoelekea katika nchi hiyo ambapo zimeshindikana kuokolewa kutokana na wavuvi wengine kushindwa kwenda baharini kufuatia hali mbaya ya hewa.

Amesema baadhi ya wavuvi wa Kenya wameziona maiti hizo zikiwa hazina vichwa na viungo vingine pamoja na mifuko ya unga wa ngano yenye chapa ya Azam ikielea baharini.

SMZ KUTANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBELEZI YA KITAIFA KUTOKANA NA AJALI YA KUZAMA MELI

Meli ya Mv Spice Islander

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK Ali Mohammed Shein, ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba mkubwa ulioikumba zanzibar kutokana na ajali ya meli iliyokuwa ikitokea Unguja ikielekea Pemba , iliyotokea usiku wa kuamkia leo.

 

Akitoa taarifa hiyo mbele ya vyombo vya habari leo jioni, huko Ikulu mjini Zanzibar DK Shein amesema Serikali inatangaza siku tatu za maombolezo kuanzia kesho tarehe 11 September, aidha  katika kipindi hicho sherehe na tafrija zote hazina budi kusitishwa sambamba na bendera kupepea nusu mlingoti.

 

Akielezea mikakati ya Serikali katika msiba huo amesema serikali itashughulikia kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwatambua waliofariki,kuwasaidia waliookolewa na waliopata maumivu, itashughulikia maziko kwa wale wote waliofariki kwa wale watakao tambuliwa.

 

Aidha DK Shein amesema kwa wale ambao hawatatambuliwa na jamaa zao Serikali itachukua jukumu la kuwazika  katiaka lililotengea huko KAMA wilaya ya Magharibi Unguja.

 

Rais alivipongeza vikosi vya ulinzi kwa kazi nzuri waliofanya katika harakati za uokozi wakishirikiana na Wananchi, pamoja na vyombo vya habari ambavyo vimefanya kazi ya ziada ya kuwajuulisha wananchi matokeo yote ya ajali hiyo.

 

Aliwataka wananchi wote na zaidi waliofiwa kuwa wastahamilivu kwa msiba huo uliowafika na waone kuwa hayo ni majaala ya Mwenyezi Mungu.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, mara baada ya kuzungumza na vyombo vya habari alitembelea eneo la Maisara ambapo maiti za wahanga hao wa ajali ya meli wanapofikia ili kutambuliwa na jamaa zao.

 

Wakati huo huo mpaka hivi sasa watu wapatao 620 wameokolewa wakiwa hai na watu 189 wamefariki dunia hata hivyo hali ya uokozi inaendelea.

BAADHI YA MAJINA YA WATU WALIONUSURIKA KATIKA AJALI HIYO

 

Ali kassim ali 14 bopwe wete

Masoud juma masoud  19 bopwe wete

Masoud ali hamad 14 wete

Rashid said khalfan wete 58

Mohd Khalid chake

Khamis kombo wete

Nassor mmanga wete

Omar juma khatib 22 mtambwe

Khamis kombo wete 33

Abdall nahoda gando 16

Rashid assaa

Nasor mmanga wete

Omar ali khamis – anani

Suleiman juma hamadi –jangombe

Khamis

Salma Rashid ali –dar

Hamri hamad

Makame sharif –kitope

Saleh jabir –pandani

Ali musa ali –kojani

Hassan vuai –gando

Ali khamis juma-kipangani

Salim hatib –shengejuu

Issa hamad juma –mtoni-kiwani

Hamdfan nahoda – mianzini

Khamis ali seif –dar

Ayami khamis – Zanzibar

Khamis jabu –konde

Hemedi

Nasra muhsin –dar

Issa ali omar –chake

Moza Rashid – dahanasa

Abdalla Othman – uwandani

Yusu fakii – mwanyaya

Swabra – wete

Khairat –wete

Safia – magogoni

Maryam murad –tanga

Nassor hamad – polisi chake

Khamis omar mbaruk – kambini

 

 

 

 

 

AJALI YA MELI YATOKEA ZANZIBAR, WATU KADHAA WAFARIKI DUNIA, JUHUDI ZA UKOZI ZINAENDELEA

Eneo la rasi ya Nungwi

Baadhi ya mili ya watu waliozama kwenye meli ya abiria na mizigo ya Spice iliyokuwa ikitokea Unguja kwenda Pemba imeanza kuletwa nchi kavu katika bandari ya Nungwi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye eneo la tukio vikosi vya ukozi vya KMKM pamoja na vyombo vingine vya wananchi vinaendelea na shughuli za ukozi.

Akizungumza na vyombo vya habari naibu waziri wa miundo mbinu na mawasiliano Issa Haji Gavu amesema vyombo vya uokozi vimeondoka bandari ya Malindi kuelekea katika eneo la tukio.

Gavu amesema msiba huo ni wa kitaifa na kuwataka wananchi kuendelea kuvuta subra na serikali itatoa taarifa rasmi juu ya maafa hayo.

Hata hivyo idadi ya watu waliokuwemo ndani ya meli hiyo na walionusurika bado haijafahamika, lakini baadhi ya viongozi wa serikali waliozungumza na vyombo vya habari wamesema watu kadhaa wamefariki dunia.

Meli hiyo ya Spice imezama usiku wa manane katika mkondo wa Nungwi na chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Wananchi wa Tanzania wameingiwa na simazi kutokana na kuguswa na msiba huo

        Taarifa za hivi karibuni zinasema meli hiyo inaendelea kukokowata na maji na mawimbi ya bahari ikielekea katika mkoa wa Tanga

NEW  NEW  NEW

Meli ya LCT  SPICE ISLANDERS imebiruka na kuzama katika Bahari ya Hindi katika Pwani ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja ikielekea Pemba.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Ussi amesema tukio hilo limetokea saa 8:30 za usiku ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba abiria 610 pamoja na mizigo.

Naibu Waziri huyo amesema meli hiyo imeondoka katika Bandari ya Malindi Unguja ikiwa katika hali ya uzima,lakini katikati ya safari ikapata hitilafu na kusababisha kubiruka na hatimaye kuzama.

Hadi sasa haijaweza kufahamika idadi kamili ya watu waliofariki,lakini vyombo vya uokozi vimefika katika eneo la tukio kutoa msaada.

Naibu Waziri Issa amesema Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya usafiri  vya binafsi boti ziendazo kasi zimekwenda eneo la tukio kutoa msaada unahitajika.Jeshi la Polisi Tanzania imetuma  Helkopta yake kwenye eneo la tukio.

Awali, amesema Mamlaka zinazohusika zilipata taarifa za kuzama kwa meli hiyo baada ya Meli ya Mv Jitihada inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuripoti kuzama kwa meli ya Spice Islanders ambayo ililazimika kukatisha safari yake kuelekea Kisiwani Pemba na kwenda kwenye tukio.

Serikali imesema taarifa zaidi zitakuwa zikitolewa na wananchi wameombwa kuwa watulivu.

 

TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR KUHUSU AJALI YA MELI

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein ametoa salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa kufuatia ajali ya meli ya Spice Islander na kusababisha watu kadhaa kufariki dunia.

Akizungumza katika eneo la kupokelea majeruhi na maiti wa ajali hiyo huko Nungwi amesema msiba huo ni mkubwa na umegusa taifa na wananchi wote wa Zanzibar.

Hivyo amewataka ndugu, jamaa na wananchi kwa ujumla kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki cha msiba.

Dr. Shein amesema serikali imeandaa utaratibu wa kuwahudumia waliokufikwa na maafa hayo na wale waliopoteza maisha, serikali itafanikisha mazishi yao.

Hata hivyo Dr. Shein amewapongeza wananchi wa kijiji cha Nungwi waliochukua hatua za awali za kuokoa maisha ya watu.

Aidha Dr. Shein amevitaka vyombo vya habari kutoa habari zenye usahihi ili kuwasaidia wananchi kupata taarifa za maafa hayo kwa usahihi.

Taarifa za hivi karibuni meli hiyo iliyokuwa na zaidi ya watu 610 hadi sasa watu 260 wameokolewa wakiwa hai.