Baadhi maiti za watu zinazosodikiwa kutoka kwenye meli ya Spice Islander iliyozama mwishoni mwa wiki iliyopita zimeanza kuonekana katika mwambao wa pwani ya Kenya.

Akizungumza na Zenji Fm radio mkaazi wa kijiji cha Moa, Tanga Bakar Bunda amesema zaidi ya maiti sita zimeonekana zikielekea katika pwani ya kijiji hicho kilichokuwa karibu na Kenya.

Amesema kitambulisho chenye jina la Masoud Shaaban Hamad mkaazi wa Mtambwe kimeokotwa kikiwa ndani ya begi dogo na wavuvi wa kijiji hicho

Aidha Bunda amesema wamepata habari kutoka nchini Kenya kuna maiti nyingine zinazoelekea katika nchi hiyo ambapo zimeshindikana kuokolewa kutokana na wavuvi wengine kushindwa kwenda baharini kufuatia hali mbaya ya hewa.

Amesema baadhi ya wavuvi wa Kenya wameziona maiti hizo zikiwa hazina vichwa na viungo vingine pamoja na mifuko ya unga wa ngano yenye chapa ya Azam ikielea baharini.

Advertisements